38 waunda timu ya Taifa kuogelea

Muktasari:

  • Baadhi ya wachezaji walichaguliwa ni Natalia Ladha, Sydney Hardeman, Sophia Latiff, Charlotte Sanford Maia Tumiotto, Chichi Zengeni, Isabelle Powell na Avalon Fischer.

Dar es Salaam. Waogeleaji 38 wamechaguliwa kuunda timu ya Taifa ya kuogelea kwa ajili ya mashindano ya Afrika ya Kanda ya Tatu (Cana Africa zone 3) yaliyopangwa kufanyika Kenya.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro alisema wachezaji wote waliofanya vizuri katika mashindano ya Taifa wamechaguliwa.

Itatiro alisema wachezaji wanaosoma na kuogelea nje ya nchi pia wamechaguliwa ili kujenga timu imara yenye lengo la kurejesha ubingwa wa mashindano hayo waliopoteza mwaka jana nchini Sudani. Tanzania ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo mara mbili mfululizo Rwanda mwaka 2016 na 2017 yaliyofanyika nchini.

Baadhi ya wachezaji walichaguliwa ni Natalia Ladha, Sydney Hardeman, Sophia Latiff, Charlotte Sanford Maia Tumiotto, Chichi Zengeni, Isabelle Powell na Avalon Fischer.

Wengine Kayla Temba, Natalie Sanford, Niamh Powell, Anna Guild ,Sonia Tumiotto, Smriti Gokarn, Sylvia Caloiaro na Maya Somaia.

Wavulana ni Romeo Asubisye, Ezra Miller, Sahal Harunani na Delbert Ipilinga, Aravind Raghavendran, Juddah Miller, Delhem Rashid, Joshua Van Schalkkwayk, Terry Tarimo, Peter Itatiro. Christian Shirima, Khaleed Ladha, Caleb O’ Sullivan, Delvin Barick na Isam Sepetu.