Mtanzania kuinoa timu ya Afrika

Muktasari:

Mashindano hayo yatafanyika katika mji wa Orlando.

KOCHA Mtanzania, Bahati Mgunda amechaguliwa kuwa kocha wa timu ya Afrika kwenye mashindano ya dunia ya mpira wa kikapu ya vijana chini ya miaka 16 .
Mgunda atakainoa kikosi hicho kinachojumuisha wachezaji kombaini kotoka nchi za  Misri, Nigeria, Senegal, Cameroon, Mali, Msumbiji na DR Congo kwenye mashindano ya dunia yatakayoanza Agosti 6 hadi 11 nchini Marekani.
Mashindano hayo yatafanyika katika mji wa Orlando.
Akizungumzia nafasi hiyo, Mgunda amesema ni ya pekee kwake na fursa kwa Tanzania kujitangaza katika mashindano hayo makubwa ya vijana.
"Pamoja na kwamba Tanzania hatuna mchezaji aliyejumuishwa kwenye timu ya kombaini ya Afrika, lakini nafasi ambayo NBA imeitoa kwa Tanzania ni ya pekee," alisema Mgunda.