MwanzoContactsEmail
Home Habari Uchumi na Biashara Wakaguzi waenda Singapore kuchunguza miradi hewa ya TBS
BOOKMARK THIS PAGE
Wakaguzi waenda Singapore kuchunguza miradi hewa ya TBS  Send to a friend
Tuesday, 21 February 2012 20:18

Patricia Kimelemeta

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imetuma wakaguzi kwa ajili ya kukagua ofisi za ukaguzi wa magari nje ya nchi zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC); Fedha na Uchumi; na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) kudai kuwa Mkurugenzi wa TBS,Charles Ekelege, aliwasilisha taarifa za uongo kwamba Tanzania ina ofisi ya ukaguzi wa magari nje ya nchi wakati siyo kweli.  

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema kutokana na tuhuma zenyewe kuhusisha nje ya nchi, ofisi yake inalazimika kutuma wakaguzi ili kufanya uchunguzi na kuhakiki ukweli kuhusu tuhuma hizo, jambo ambalo anaamini linaweza kupata taarifa sahihi.

“Tumelazimika kutuma wakaguzi nje ya nchi kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kukagua ofisi za ukaguzi wa magari hayo, hii itasaidia kupata taarifa sahihi kuhusu tuhuma hizo na ukweli wa mambo yenyewe, jambo ambalo linaweza kurahisisha upatikanaji taarifa sahihi za madai hayo,” alisema Utouh.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, ofisi yake itakuwa makini katika suala hilo ili uamuzi utakaotolewa na Serikali usiweze kulalamikiwa na kuonekana umetokana na uonevu.  Kwa mujibu wa Utouh, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo, aliwasilisha taarifa hizo mwishoni mwa wiki iliyopita na kwamba, tayari wameanza kuifanyia kazi ili kupata ukweli wa madai hayo.

“Siwezi kumuonea mtu katika hili, ndiyo maana naifanya kazi ya kuhakiki kwa umakini zaidi il taarifa yake iweze kukamilika na uamuzi utakaotolewa usiwe wa kumuonea mtu,”alisema. Hata hivyo, kamati hizo zilitoa mapendekezo yao ya kumtaka CAG kuchunguza tuhuma hizo kipindi cha mwezi mmoja kwa kulinganisha na maelezo yatakayotolewa na Mapunjo.

Januari 27, mwaka huu POAC na PAC ilibaini kuwapo kwa tuhuma hizo zilizoelekezwa kwa mkurugenzi huyo na kumtaka asimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #3 2012-02-22 11:39
Huu ni utani sasa, ubalozi upo na maofisa makini sana waulizeni watawaambia ukweli. kusafiririsha maofisa wa serekali mpaka huku ni ufajaji mwingine tu. Tnzania bwana kweli shamba la bibi.
Quote
 
 
0 #2 2012-02-22 08:58
Hii ndio tanzania!c ajbu mkurugez huyu kapitia Jkt kupewa maadil na uzaleo wa nchi.ninacho weza sema nchin kila mtu anawaza kujnufaisha mwenyewe.
Quote
 
 
+1 #1 2012-02-22 08:23
hivi ofisi ya CAG ni ya zima moto wa Bunge...............mbona haijitumi yenyewe?
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner