
| Kesi ya Kafulila kutajwa Machi 15 | Send to a friend |
| Tuesday, 21 February 2012 20:17 |
|
KESI ya kupinga kuvuliwa uanachama inayomkabili Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila na wenzake saba imepangwa kutajwa Machi 15, mwaka huu. Kafulia na wenzake kupitia kwa wakili wao, Daniel Welwel, walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya NCCR-Mageuzi akipinga uamuzi wa chama hicho kumvua uanachama. Licha ya Kafulila, walalamikaji wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu 2010, Wakili Hashimu Rungwe, Mbwana Hassan, Henry Mapunda, Kayombo Kabutali, Sued Omar, Diamond Mwasampeta na Issa Hussein. Kesi hiyo namba 218/2011 ilitarajiwa kuanza kutajwa jana, lakini iliahirishwa kutokana na kutokuwapo kwa Jaji anayeisikiliza, Alice Chingwile. Akiahirisha kesi hiyo, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alisema Jaji Chingwile yuko kwenye kesi nyingine za mauaji mkoani Morogoro na kwamba, kesi hiyo itatajwa Machi 15, mwaka huu. Katika kesi ya msingi, Kafulila anaomba mahakamakuitengua uamuzi wa Halmashauri Kuu (Nec) chama hicho wa kumvua uanachama, uamuzi ambao utekelezwaji wake unamfanya apoteze sifa za kuwa mbunge. Sambamba na kesi hiyo ya msingi, pia Kafulila aliwasilisha maombi akiomba mahakama iamuru utekelezaji wa chama hicho kumvua uanachama usitishwe hadi kesi ya msingi itakapomalizika. Kutokana na maombi hayo, Desemba 27, mwaka jana Jaji Chingwile alikiamuru NCCR- Mageuzi kutochukua hatua nyingine zozote dhidi ya Kafulia na wenzake hadi kesi yao ya msingi itakapoamriwa. Desemba 18, mwaka jana Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimvua uanachama Kafulila, siku kumi baada ya kumwengua kwenye nafasi ya Katibu mwenezi wa chama hicho kwa tuhuma za kutoa siri za chama. Mbali na Kafulila, wengine waliovuliwa uanachama wa chama hicho siku hiyo ni Rungwe, Mbwana Hassan Yotham Lubungila, ambao wote walikuwa ni wajumbe wa halmashauri kuu. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Prof Mwandosya aapishwa waziri kazi maalum
- Katiba Mpya: Wananchi Makambako waapa, iwe jua au mvua lazima watoe maoni yao
- Mchakato wa Katiba: Nahodha yupi aaminike? 1
- Wanavyosema wanasiasa kuhusu Katiba mpya
- Serikali inasita nini kutumia Kiswahili kufundishia shule za sekondari?
- Jamii inaweza kuleta mabadiliko katika elimu
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments