MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
BOOKMARK THIS PAGE
Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto  Send to a friend
Tuesday, 20 April 2010 22:30

Patricia Kimelemeta na Voina Maganda
SERIKALI, ambayo inahaha kujaribu kuzuia mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kufanyika kuanzia Mei 5, imetangaza nyongeza ya asilimia 100 ya mishahara ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na kuahidi kutangaza mishahara ya watumishi wa umma kabla ya Mei mosi mwaka huu.

Lakini Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limesema hatua hiyo haitabadili msimamo wake kwa sababu inahisi ni ya kisiasa hivyo hawatatangaza kusitisha mgomo wao hadi madai yao yote  yatekapotekelezwa.

Madai yaliyoifanya Tucta itangaze mgomo huo ni pamoja na nyongeza ya kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma hadi kufikia Sh315,000, kupanua wigo wa kodi ili kumpunguzia mfanyakazi mzigo wa kulipa kodi na makato kwa ajili ya mifuko ya hifadhi za jamii.

Lakini jana, serikali iliamua kuweka kwanza kiporo madai hayo ya Tucta na kutangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa sekta binafsi.

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa ongezeko hilo la mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi, liwanagusa wafanyakazi wote katika sekta hiyo.

Kwa tamko hilo la serikali lililotolewa kwa mamlaka aliyonayo waziri mwenye dhamana kifungu namba 41 (1) cha sheria ya ajira namba 7 ya mwaka 2004, mishahara ya watumishi wote wa sekta binafsi iliyotangazwa Oktoba 8 mwaka 2007 na aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana  John Chiligati, sasa italipwa mara mbili.
Chiligati alitangaza viwango hivyo vya mishahara ambavyo vilianza kutumika Novemba mwaka 2007 baada ya mvutano mkali kati yake na Tucta.

Viwango vya zamani vya kima cha chini kisekta pamoja na viwango vipya sasa vimetangazwa vitumike ni kutoka Sh65,000 hadi Sh130,000) kwa sekta ya kilimo, meli za mizigo na za abiria (Sh225,000 hadi Sh450,000), meli za uvuvi za ndani (Sh196,000 hadi Sh392000), makuli na wajenzi wa meli (Sh300,000 hadi Sh600,000).

Wafanyakazi wa majumbani wapo katika makundi matatu; wanaofanya kazi kwa mabalozi (Sh90,000 hadi Sh180,000),wanaowafanyia maofisa wanaolipiwa huduma hiyo na waajiri wao (Sh 80,000 hadi Sh160,000) na wengine (Sh65,000 hadi 130,000).

Wanaofanya kazi mahotelini (Sh150,000 hadi Sh300,000), hoteli za kitalii na hoteli za kati (Sh100,000 (200,000) na hoteli ndogondogo, baa, nyumba za wageni na migahawa (Sh80,000 hadi Sh160,000).
Katika sekta ya madini, upande wa migodi mikubwa, wafanyakazi wanalipwa Sh350,000 na hivyo watatakiwa kulipwa Sh700,000, lakini waajiri wanaoshughulika na machimbo ya chumvi au chokaa waliwekwa kwenye kundi la viwanda vidogo kwa kuwa uwezo wao ni mdogo.

Viwanda vidogo itakuwa kutoka Sh80,000 hadi 160,000, ulinzi binafsi, kampuni za kigeni (Sh105,000 hadi Sh210,000) na kampuni nyingine (S 80,000 hadi Sh160,000), sekta ya biashara na viwanda inayojumuisha mabenki, kima cha chini kilikuwa Sh150,000 na sasa kitatakiwa kiwe Sh300,000.

Sekta ya afya imegawanywa katika makundi mawili yanayohusisha hospitali kubwa na maduka ambayo mshahara wake wa kima cha chini ni Sh120,000 na sasa itakuwa Sh240,000) na hospitali ndogo na zahanati (Sh80,000 hadi Sh160,000).

Wafanyakazi wa huduma za anga mshahara wa kima cha chini ulikuwa Sh350,000 na sasa utakuwa Sh700,000,  wasafirishaji wa mizigo (clearing and forwarding) ilikuwa Sh230,000 na sasa itakuwa Sh460,000), mawasiliano ya simu Sh 300,000 (600,000), usafiri wa nchi kavu (makondakta na madereva) sh 200,000 (400,000).

Wafanyakazi katika vyombo vya habari wamegawanywa katika makundi mawili. Katika kundi linalohusisha vyombo vinavyojiendesha kibiashara, mshahara wa kima cha chini utabadilika kutoka Sh 250,000 hadi Sh500,000.
Vyombo vingine ni vile visivyojiendesha kibishara kama vile vinavyorusha matangazo ya kidini, ambavyo kima cha chini kilikuwa ni Sh150,000 na sasa kitakuwa Sh300,000.

Wakati serikali ikitangaza viwango hivyo vya kima chini cha mshahara mwaka 2007, iliweka wazi kwamba mwajiri haruhusiwi kulipa chini ya kiwango lakini anaweza kukiongeza kwa kadri anavyopenda ili kuboresha hali za wafanyakazi wao.

Hata hivyo, viwango hivyo vilizua mtafaruku kwa waajiri wengi wakidai wakivitekeleza watafilisika kutokana na biashara kuwa ngumu na hasa ikizingatiwa wakati huo gharama za mafuta zilipaa na kukawa na wasiwasi pia ya dunia kukumbwa na uhaba wa chakula.

Kwa kujua yaliyotokea kwenye sekta binafsi baada ya kutangaza viwango vipya mwaka 2007, Profesa Kapuya aliwataka waajiri wajitahidi kuvitekeleza kama vilivyotangazwa na serikali ili kuepusha migogoro sehemu za kazi.
Aliigeukia Tucta akisema ilitoa mapendekezo saba ya kuitaka serikali kuyatekeleza kwa ajili ya kuondoa mgogoro huo na yoye yametekelezwa.

Alisema tayari serikali imeridhia mapendekezo hayo na kilichobaki ni kuendelea na taratibu za mazungumzo hayo ili kuendeleza mchakato huo ikiwa ni pamoja na kutangaza siku ya kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mishahara.

Kapuya  alisema serikali pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi walikaa kwenye kikao cha utatu kilichoitishwa na Baraza la Upatanishi (Lesco), ili kujadili hoja hizo saba.
Kuhusu wafanyakazi wa serikali, alisema wataongezewa mishahara hiyo baada ya kutolewa notisi kwenye gazeti la serikali hivi karibuni ili waweze kutangaza ongezeko hilo kabla ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo hufanyika Mei Mosi.

“Tumemaliza tofauti zetu, hivi sasa tuko kwenye mchakato wa mwisho wa kumaliza mgogoro huu. Kutokana na hali hiyo wafanyakazi wa sekta binafsi watalipwa ongezeko la asilimia mia moja, wakati serikali itatangaza rasmi kuongezwa kwa mishahara hiyo kabla ya sherehe za Mei mosi. Hivyo basi tunaamini kuwa wafanyakazi wataendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Profesa Kapuya.

Kutokana na hali hiyo,  alisema Aprili 27, mwaka huu watafanya kikao ambacho kitatoa majumuisho ya suala zima la mgogoro huo pamoja na hatua zilizofikiwa juu ya maamuzi yaliyobaki.
Profesa Kapuya alisema ikiwa wafanyakazi wataaamua kuendelea na mgomo wakati muafaka wa matatizo yao umepatikana, utakuwa ni kukiuka sheria kwa sababu watakuwa wamevunja makubaliano waliyofikia kwa pamoja.
Lakini hali haikuwa hivyo kwa upande wa Tucta. Naibu Katibu Mkuu Nicholaus Mgaya aliitisha mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa mgomo upo pale pale kama ulivyopangwa.

Hata hivyo, Mgaya alisema makubalino yao na serikali ni kurudi kwenye meza ya majadiliano na sio kuzima mgomo.
Mgaya alisema kutokana na hali hiyo wafanyakazi wataendelea kushikilia msimamo wa kugoma ikiwa serikali itashindwa kuyafanyia kazi malalamiko yao kabla ya sherehe za Mei mosi.

“Tunachokitaka sisi ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanaongezwa mishahara yao,” alisema Mgaya.
Aliongeza kutokana na hali hiyo wameitaka serikali iache siasa badala yake itatue matatizo hayo kwa kutumia busara na utalaamu.

Alisema makubaliano hayo ni kurudi kwenye meza ya majadiliano wakati serikali inaendelea kurekebisha mishahara ya wafanyakazi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 21 April 2010 23:11
 

Comments 

 
+1 #43 2011-04-15 11:25
naona mmetangaza mishahara mipya kwa makundi lakini naona sisi wataalamu wa kumpyuta hamjatuweka hapo,vp mjui sisi now ndo tunarun dunia.
Quote
 
 
0 #42 2010-08-15 12:55
Yote muyaongeayo ni sahihi Lakini tunaomba ahadi ziwe za kweli sio za kisiasa tuu maana Tz siasa ipo mbele kuliko kujali wananchi wake
Quote
 
 
0 #41 2010-04-28 16:18
Jamani tumeonewa vya kutosha haswa katika sekta binafsi. Ukiangalia mishahara tunayopewa migodini ni midogo kulinganisha na kodi tunayokatwa. Exparts wanapokuja Tanzania mara nyingi wengi wao unakuta hawajui kazi tunawafundisha sie na mishahara yao wanapokea zaidi ya milioni 20. Mimi mtanzania nafanya kazi kuzidi huyo expart matokeo yake naathirika na kemikali wanazotumia kufanya blasting. Kampuni ikiona kwamba nimeumwa mwezi mmoja au miwili naachishwa kazi sababu niko unfit kufanya kazi. Malipo yake hayatoweza kunitibu hata japo kwa mwezi mmoja. Kwa mantiki hiyo basi sisi kama wafanyakazi tuwe na umoja mishahara iongezwe kwa 100% na kodi ya mapato ipunguzwe, mpaka bonus inakatwa kodi jamani! KWAKWELI TUMECHOKA KUNYANYASIKA! SERIKALI IANGALIE HILI SWALA KWA UMAKINI ZAIDI.
Quote
 
 
+1 #40 2010-04-21 21:59
Kiwango cha mshahara mimi naona ni sahihi kwa kadiri ya hali ya maisha ya sasa. Ila nina wasi wasi kidogo kuwa wengi wa wafanyakazi watapoteza kazi zao kwa sababu si wengi wa waajiri watakubali au wataweza kulipa viwango hivi vya mishahara. Lakini serikali nayo ilipe kweli viwango vya kuridhisha kwa wafanyakazi wao. Wasibane secta binafsi tu!
Quote
 
 
0 #39 2010-04-21 21:11
Watanzania tusimame imara.
Posho za wabunge, mawaziri, makatibu wakuu,n.k ni za kukufuru. Wanakula na kusaza wakati wafanyakazi ambao ni wazalishaji wanateseka.
Wafanyakazi msikubali, Tanzania ni Tajiri. Ufisadi ndo umepandisha gharama za maisha. EPA, Kagoda, Meremeta, RADar, ndege ya raisi na mengi.

Nawaomba Mwananchi Newspaper ichape haya maoni ya wananchi katika ukurasa maalumu.

Serikali ya chama hiki kinachotawala inachangiwa na Makampuni ya private seckta katika kampeni, ndo maana wanapendelea waajiri na kukandamiza wafanyakazi.
Quote
 
 
+1 #38 2010-04-21 17:03
La msingi hapa ni serikali kuangalia njia mbadala ilikuweza kumpunguzia mfanyakazi mzigo mkubwa wa kodi anaoubeba ili take home yake iongezeke. Tatizo hapa ni kodi kubwaaaa.
Quote
 
 
0 #37 2010-04-21 16:39
WATANZANIA TUAMKE WOTE KUTETEA MASILAHI YETU TUMEVUMILIA TUMECHOKA WAO HUTUNGA MISWADA NA KUJIONGEZEA MISHAHARA HUU NI U[NENO BAYA] IKIBIDI TUINGIE BARABARANI HATA TUFE LAKINI IPO SIKU ITAFAHAMIKA TUCTA MSITUANGUSHE TUPO PAMOJA TUANGALIE MIFANO YA NCHI MAJIRANI TUMESOMA LAKINI HATUJIAMINI TUNA MENGI YA KUSEMA ILA MDOMO UMEJAA MAJI KAMA TUMEAMUA KWELI NA IWE KWELI
Quote
 
 
0 #36 2010-04-21 16:29
imefika muda watanzania tujue hatuna viongozi nchi hii,itafika muda tutaomba wakoloni warudi watutawale tena,manake hata angalau infrastructures tutaziona,,hata watakuwa na huruma kwa sisi walala hoi kunyang'anywa hata kipato kidogo cha mshahara na kuzidi kukumbatia mafisadi, safari za nje kwa watendaji wa serikali kila siku,,mgomo pale pale,,,
Quote
 
 
0 #35 2010-04-21 16:05
Kwa kweli sasa wananchi wa Tanzania tumechoka serikali imeoza wananchi sasa watachukua nchi yao wenyewe mana kama ni sheria hata sasa wananchi wanachukua tena mkononi huwezi kudanganya wananchi wote wakati wote balu utawadanganya kwa muda fulani sasa muda ule wa kudanganya wananchi umekwisha. Wkubwa mmekula sana pesa za wavuja jasho hebu muone aibu hiyo kodi kubwa mnayochukua haisaidii wamanchi bali wakubwa wachache na familia zao sasa basi tumekataa amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa hali hii angalieni tunakokwenda ni kubaya comment zote hizi hakuna hata mtu mmoja anaeisema vizuri serikali ni shutuma tu. Tucta tuko nyuma yenu sisi wafanyakazi wa nchi hii KEEP IT UP tutawaunga mkono kwa mamilioni
Quote
 
 
+1 #34 2010-04-21 16:00
Hivi kwanini serikali haioni aibu kuchukua fedha kubwa kiasi hicho kutoka kwa wafanyakazi wakati wanatoa misamaha ya kodi.kusanyeni kodi yote yuone kama haitatosha.
Quote
 
 
0 #33 2010-04-21 15:59
kiukweli sera za ukandamizaji,si asa za unyonyaji na ubadhirifu kwa viongozi ndio sera ya serikali na chama tawaala.Bila shaka tukta mmelitambua tupo pamoja kwani maisha ya mtanzania yana bana hata pa kupumulia hatupaoni hivyo serikali iwe macho na ikiwezekana ipandishe mishahara hata asilimia200.
Mfano mwalimu mshahara wake ni sawa na kipaTO CHA MUUZA KARANGA AMBAYE HANA HATA PROFFESIONAL.
Inakera inaumiza mali ya mtanzania anapewa bure mgeni .
Tunajiandaa kuwaweka sawa hatutaki ubabaishaji ukweli ndo huo naufumbuzi wa suala hili uwe active vinginevyo hata kura hamtapata.

ni hayo
by peter 0757113505 :sigh:
Quote
 
 
0 #32 2010-04-21 15:41
Hii ni safi sana,lakini serikali yetu kwa nini wanataka mpaka watishiwe mgomo ndiyo wasikilize maombi ya watanzania?,halafu wizara husika wafanye ufuatiliaji maana hata wakati uliopita walitangaza viwango vya mishahara,lakin i kuna baadhi ya mashirika na makampuni yaliendelea kulipa mishahara ya chini kabisa na serikali ikiendelea kuchukua kodi kwa nini?.
Quote
 
 
0 #31 2010-04-21 15:23
Tucta msikubali kuburuzwa na siasa za serikali hii,kuweni na msimamo mpaka kieleweke.ifike mahali serikali itambue mchango mkubwa wa wafanyakazi katika nchi hii.TUMECHOKA
Quote
 
 
0 #30 2010-04-21 15:15
Mimi nadhani serikali iwe makini na hili,ongeza mishahara then punguza kodi.wafanyakazi tumechoshwa na porojo za serikali.MGOMO UBAKI PALE PALE.
Quote
 
 
0 #29 2010-04-21 14:49
My comment is
imekuwa ni mazoea kwamba watanzania wanapokuwa wanadai haki zao hakuna utekelezaji wa haraka zaidi ila wabunge ambao ni miongoni mwa watanzania wanapodai haki zao huwa zinashughulikiw a kwa haraka zaidi wazo langu viongozi wa tucta kuweni makini kushughulikia hili nawala msiwageuke watanzania kwa kupewa vijisent ili kuiuwa issue
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner