MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Mwakyusa: Tumshukurmu Mungu kwa dawa ya ukimwi
BOOKMARK THIS PAGE
Mwakyusa: Tumshukurmu Mungu kwa dawa ya ukimwi  Send to a friend
Wednesday, 14 July 2010 07:58

Leon Bahati

WAKATI wanasayansi waliogundua dawa ya Ukimwi wakiweka bayana jinsi inavyofanya kazi mwili kupambana na ugonjwa huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa amemshukuru Mungu kwa taarifa za ugunduzi wa dawa hiyo.Taarifa ya kupatikana kwa dawa hiyo zilitangazwa mwishoni mwa wiki na wanasayansi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) ya Marekani, akisema kuwa tiba hiyo inaweza kutibu ugonjwa huo hatari kwa asilimia 90, kiwango kinachoiweka dawa hiyo kwenye uwezekano mkubwa wa kupitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na hivyo kuanza kutumika rasmi.

Dawa hiyo huchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi. Chembechembe hizo zimepewa jina la kitaalamu la VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuvikabili virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90.

Habari hizo, ambazo zimekuwa gumzo duniani kote, zilimfurahisha pia Waziri Mwakyusa, wakati wasomaji wa Mwananchi walikuwa wakituma maoni yao kuzungumzia matokeo ya utafiti wa dawa hiyo, wengi wakifurahia kuwa sasa "wamewekwa huru".

Akizungumza na Mwananchi, Prof Mwakyusa alisema: "Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba wananchi wake wanapata huduma za tiba hata kama ni ghali kiasi gani.

"Kama ni kweli dawa hiyo imepatikana, ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwa Ukimwi ni ugonjwa ambao umeiathiri sana dunia."

Alisema serikali imekuwa ikitumia mamilioni ya fedha kupambana na ugonjwa huo na hivyo kuwezesha dawa nyingi ghali duniani zinazopunguza makali ya ugonjwa huo na kutibu magonjwa sugu kutolewa bure kwa wananchi.

Alitoa mfano wa dawa hizo kuwa ni zile za kutibu malaria maarufu kwa jina la Alu, dawa za kutibu kifua kikuu na zile za kupunguza makali ya ukimwi.

"Na hata kama hizo za kutibu ukimwi zitakuwa zimepatikana, bado mataifa makubwa yana wajibu wa kuhakikisha zinaweza kuwafikia kirahisi watu katika nchi masikini," alisema Profesa Mwakyusa.

Kwenye chumba cha habari cha Mwananchi, wasomaji walikuwa wakipiga simu kuelezea kufurahishwa na taarifa hiyo huku wengine wakitoa maoni yao kwenye mtandao, wengi wakisifu matokeo ya utafiti huo na wengine wakisema kuwa bado kuna safari ndefu.

Nchini Marekani, wanasayansi wa Niaida waliweka bayana namna dawa hiyo inavyoweza kufanya kazi katika mwili wa binadamu wakati wa kupambana na ugonjwa huo hatari.

Niaida imetoa taarifa hiyo kufuatia taarifa iliyotangazwa wiki iliyopita kwamba wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinaweza kutumika kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa asilimia 90.

Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alisema katika taarifa kwenye mtandao wa taasisi hiyo kwamba dawa waliyoigundua siyo ya kwenda kuua moja kwa moja virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa binadamu, bali ni kuchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi.

Dk Fauci alisema kuwa chembechembe hizo, VRCO1 na VRCO2, zinapambana tu na virusi vya Ukimwi jambo ambalo linawapa faraja kuwa chembechembe hizo haziwezi kusababisha madhara kwa mwili wa binadamu.

Mtaalamu huyo alieleza kwamba kinachofanywa na chembechembe za kinga za VRCO1 na VRCO2 kwenye mwilini binadamu, ni kuvibana virusi vya Ukimwi na kuvifanya vishindwe kuendelea kushambulia seli nyeupe za damu.

Kwa kawaida virusi vya Ukimwi hushambulia seli nyeupe za damu ambazo ni muhimu katika kusaidia mwili kujikinga na maradhi ama kwa jina jingine la kitaalamu CD4, ambako virusi vya Ukimwi hugeuza kuwa makazi yake.

Kila seli nyeupe inayoshambuliwa, wataalamu wanasema, hufa baada ya kutumika kuzalisha virusi wengine na mzunguko huo huendelea hadi mwili unapojikuta umepungukiwa na kinga kiasi cha kushindwa kuhimili vishindo vya maradhi ya kawaida.

Wataalamu wanasema hali hiyo ndiyo inayomfanya mwathirika wa Ukimwi kufa.

Dk Fauci alisema Chembechembe za  VRCO1 na VRCO2 hubana mashambulizi ya virusi vya Ukimwi kiasi cha kushindwa kuendelea na uharibifu wa CD4.

Kwa sababu hiyo, alisema dawa watakayoitoa katika hatua ya kwanza kupitia chanjo ni kwa ajili ya kuufundisha mwili namna ya kutengeneza chembechembe za VRCO1 na VRCO2 ambazo zitakabiliana na virusi wa ukimwi.

"Kwa kutumia teknolojia tuliyogundua tutatengeneza aina ya chanjo ambayo kazi yake itakuwa ni kuufundisha mwili namna ya kutengeneza chembechembe za kinga aina ya VRCO1 ambazo zitakuwa na uwezo wa kupambana na virusi vya ukimwi," alisema Dk Fauci.

Wanasayansi wa Niaida walioshiriki kwenye utafiti huo ni Dk Peter Kwong, Dk John Mascola na Dk Gary Nabel.

Wataalamu hao wanaelezewa kuwa waliongoza timu mbili ambazo ziliendesha utafiti huo ambao ulihusisha damu za waathirika kutoka karibu kona zote za dunia.

“Tulitumia utaalamu wetu kujenga mazingira yote ya virusi wa Ukimwi na ndio tukaweza kufahamu namna ya kujenga mazingira ya kudhibiti virusi hivyo," alisema mmoja wa wajumbe wa jopo la madaktari hao waandamizi, Dk Nabel.

Aliongeza: "Haikuwa kazi rahisi kwa sababu virusi vya Ukimwi vina tabia ya kujibadilishabadilisha. Na hii ndiyo imekuwa ikiwapa taabu wataalamu wengi katika kupata tiba.

"Kujibadilishabadilisha huko kumefanya dunia kuwa na aina mbalimbali za virusi. Utafiti wetu umewezesha kutengeneza mazingira ya kukabiliana na namna zote za virusi kuweza kujigeuzageuza."

Isitoshe Dk Nabel alisema chembechembe za kinga za VRC01 na VCR02 zina uwezo wa kupenya mazingira yote ambayo CD4 za mwili zinaweza kupatikana.

Dr Mascola yeye alielezea ufanyakazi wa VCR01 na VCR02 kuwa ni wa ajabu kwa sababu zinapambana na aina zote za utendaji wa virusi vya Ukimwi.

Wataalamu hao walisema VRC01 na VRC02 haviingilii itendaji kazi wa seli kwa namna yoyote ile bali kukabiliana na harakati za virusi vya ukimwi.
Dk Faci alisema haya ni maendeleo mazuri katika kipindi hiki ambacho waathirika wa Ukimwi wamekuwa wakitumia tu dawa za kutuliza makali ya virusi.

Maelezo ya wataalamu ni kwamba anayetumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi atatumia maisha yake yote na huwa hazitibu.
Lakini katika ugunduzi wa dawa yao, Dk Fauci alisema binadamu atapatiwa chanjo hiyo kwa mara moja na itatosha kabisa kuuweka mwili wake katika kuandaa majeshi ambayo yatakabiliana na virusi.

Tayari baadhi ya wataalamu wamekiri kuwa ugunduzi huo wa Niaida umeleta mapambazuko ya tiba ya ugonjwa huo na mojawapo ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani ambayo imesema kuwa dawa hiyo haitakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.

Dk fauci amewahi kuongoza Taasisi ya Taifa ya Afya (NIH) ya Marekani kuanzia mwaka 1968 na kuaniza 1974 aliteuliwa kuongoza vitengo mbalimbali maalumu vya tiba nchini humo.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha utafiti wa tiba cha Niaida mwaka 1980 na mwaka 1984 akateuliwa kuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo, nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 15 July 2010 08:17
 

Comments 

 
0 #55 2010-07-21 14:02
Ndugu zangu Watanzania tumshukuru Mungu kwani yeye ndio, muweza wa yote,swala kutupatia dawa sio mchezo,ila tusijisahau sana kwa kigezo kuwa dawa imepatikana sasa ndiyo tufanye ngono zembe ,haitopendeza jamani,mie nawaombeeni kwa mungu muendeleze yalo mema tu.MWISHO TUSISAHAU KUMCHA MUNGU KWA KILA JAMBO,KWANI HAKUNA LINALOSHINDIKAN A KWAKE YEYE. BE CAREFUL AIDS IT KILLS.REMEMBER THAT PREVENTION IS BETTER THAN CURING.THANK YOU.
Quote
 
 
0 #54 2010-07-15 12:44
kwa chochote tukifanyacho kikifanikiwa tunasema 'asante mungu'. kila mtu anajua kuwa huwa halali halafu anamtegemea mungu amshushie ili akishamshushia ndo aseme 'nashukuru mungu'. hata prof anajua hili. pia wote twajua tunaposalia chakula tunasema 'asante mungu'. sa unayemlaumu prof kwa kusema asante mungu (kama dawa imepatikana kweli) una maana gan? au kwa ukimwi asingesema hivyo?
mi naomba God dawa iwe imepatkana kweli
Quote
 
 
0 #53 2010-07-15 10:36
ALHAMDULLILAH.i knew from the start that the cure ipo.qur an imeandika kila ugonjwa una dawa yake.why hiv isiwepo dawa yake.jamani haya ni mafanikio makubwa.Tumuombe mungu atufunilie zaidi juuu ya dawa hii na huku afrika tuje tuipate.
Quote
 
 
0 #52 2010-07-15 06:56
sasa wewe godfrey ulikuwa unatakaje? kwani unaonekana kuwa na bifu na hao wagunduzi embu jaribu wewe halafu ufikie hat asilimia 50 tu uone tutakavyokusifu , na kama mimiea ipo bongo embu fanya basi tukuone, its just roho mbaya hiyo. hata tufanye nini hatuwawezi wazungu just imagen wamegundua vingapi? kazi yetu wabongo ni copy an paste tu no addtion, best kuwa makini mzungu muache na still mpaka leo wanatutawala neo colonialsm, mmm mwenzetu badilika its bad usipo wapa heko watu waaojaribu kuokoa maisha hata ya watoto wetu tumboni, what i can say GOD release power to those person and protect them till day of implimentation.
Quote
 
 
0 #51 2010-07-15 05:38
Hiyo dawa mpaka ifikie wakati wa kutumika si leo wala kesho. Jamani ukimwi upo jihadharini nao. Na nyie mnaotukanana katika magazenu kuweni na hekima kwani watu wanatamani kusoma maoni yanayotoa changamoto katika jamii. Baadhi ya wanaosoma magazeti kama hya ni watoto wetu sasa mtu anapoandika mambo ya ajabu ajabu ni vema haipendezi jamani. Tuheshimiane!
Quote
 
 
0 #50 2010-07-15 05:31
Ninaungana na awatoa maoni wengine. Serikali yetu itambue umuhimu wa kutumia taasisi zake za tafiti mbalimbali ili kuboresha afya, kilimo, makazi, nishati, nk kwa kutenga fedha za kutosha kwa jili hiyo badala ya kutenga fedha nyingi kwa kunywea chai na vitafunwa, poshoza safari, na ununuzi wa magari ya kifahari!
Quote
 
 
0 #49 2010-07-15 04:45
Quoting Godfred Kakengi:
Kwanza nasikitishwa na maneno ya "Jamani tumshukuru Mungu". Mungu gani atakuletea maendeleo au tiba ya magonjwa. Ni sisi wenyewe na akili yetu na wala hakuna hayo mambo ya Mungu. Kwa nini tunasubiri kutengenezewa dawa na hawa wakoloni wakati sis tuna kila uwezo wa kufanya hivyo? Wasomi wa mambo ya madawa tunao, serikali tunayo! kwa nini tunawalamba lamba hawa. Hata hiyo mimea ya kutengeneza hiyo kinga inawezekana inatokea kwetu!
Mambo ya kuwaabudu hawa watu inabidi tuyaache na tuanze kufanya mambo yetu bila ya kuingiliwa na wao. Tufanye kama India walivyofanya, kufunga mipaka na tuanze kugundua mambo yetu kama tulivyofanya huko Misri kabla ya kuvamiwa na wegriki na waarabu.

watu walo[NENO BAYA]a mambo misri walikuwa ni waafrica wenye asili ya kiarabu hakuan mtu mweusi ambaye aligundua kitu wacha u[NENO BAYA] wewe mpogoro ..ndio kweli kila kitu kinatoka barani kwetu africa ...mungu alitupa kila kitu akatunyima akili ukipenda usipende hawa watu wametuzidi kila kitu na wao wanaupendo tofauti na sisi weusi tunaroho mbovu na hatufiki sehemu yoyote siunaona dada zako na kaka zako weusi mrekani hawana tafauti na wewe unayeishi gongo la mboto wakippata pesa basi wanakwenda kutia meno almasi..baada ya miezi mine au mitatu majalala same shit na hao viongozi wenu wa[NENO BAYA] pamoja na wewe wakiafrica
Quote
 
 
0 #48 2010-07-15 03:29
Hii sasa kiruwe ruwe,.. dawa ya ukimwi imeaptikana? nani anauhakika huo? nani amajaribu na sasa huoy hai amepona? wantazania wenzangu tuendelee kutumia zana vywtu.. wanasayansi wajaribu wenyewe!!! lol!!
Quote
 
 
+1 #47 2010-07-15 02:53
Nyie wachangiaji wote hamuelewi mnayoyaongea. Si kwamba [NENO BAYA] la hasha bali mmeongea kulingana na upeo wenu ulivyo lakini mh. waziri yuko sawa kabisa kwa kila aliloliongea.

Poleni lakini mtaelimika hivi karibuni.
Mungu anawapenda sana na kwa wewe Godfred hapo juu hatakama humuamini yeye anakuamini so usijali.
Quote
 
 
-1 #46 2010-07-14 23:12
Kwanza nasikitishwa na maneno ya "Jamani tumshukuru Mungu". Mungu gani atakuletea maendeleo au tiba ya magonjwa. Ni sisi wenyewe na akili yetu na wala hakuna hayo mambo ya Mungu. Kwa nini tunasubiri kutengenezewa dawa na hawa wakoloni wakati sis tuna kila uwezo wa kufanya hivyo? Wasomi wa mambo ya madawa tunao, serikali tunayo! kwa nini tunawalamba lamba hawa. Hata hiyo mimea ya kutengeneza hiyo kinga inawezekana inatokea kwetu!
Mambo ya kuwaabudu hawa watu inabidi tuyaache na tuanze kufanya mambo yetu bila ya kuingiliwa na wao. Tufanye kama India walivyofanya, kufunga mipaka na tuanze kugundua mambo yetu kama tulivyofanya huko Misri kabla ya kuvamiwa na wegriki na waarabu.
Quote
 
 
+1 #45 2010-07-14 18:50
Inshallah Mungu ataleta nusurah yake. God is great.
Quote
 
 
0 #44 2010-07-14 17:41
jamani tuwapongeze na kuwaombea kuongezea uwezao pia tuendeleze sala zetu ili watanzania waliowengi wasiendeleeee kupoteza uhai wa wazazi wao kama makete na bukoba amin
Quote
 
 
0 #43 2010-07-14 17:30
Yap. mapambano yaendelee kama kawa. sasa kama virus wakishambuliwa wakapungua kiasi cha kutoonekana kwenye vipimo si itakuwa vigumu kujua nani yupo salama? Akikuchangia damu je? Naona tusilegeze msimamo kukabiliana na ukimwi hata kama yapo matumaini ya tiba.
Quote
 
 
0 #42 2010-07-14 16:37
jamani hizo ni taarifa za awali,cha msingi hawa watafiti tuwape nafasi ya kushughulika zaidi na hicho walicho anza nacho na si kubeza tuu wakati sisi tumeshindwa!!je tumesahau kwamba `plague disease`{tauni} ilichukuwa zaidi ya miaka 300 bila dawa na badaye kikaeleweka?Tatizo waafrika wavivu kusugua vichwa!tuache wanaoweza waendelee!
Quote
 
 
+1 #41 2010-07-14 16:23
Ndugu zangu Wantania, msibadili mwenendo hiyo ni asilimia 90 si asilimia 99, kwa niyo " Tafadhali jikinge na UKIMWI" hatari.Mh.usiwepa moyo wapenda Ngono.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner