MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa IKULU yajitenga na ripoti ya Mwakyembe
BOOKMARK THIS PAGE
IKULU yajitenga na ripoti ya Mwakyembe  Send to a friend
Tuesday, 21 February 2012 20:19

Leon Bahati
OFISI ya Rais (Uhusiano na Uratibu), imejitenga na taarifa tata za ripoti kuhusu ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, kama unatokana na kulishwa sumu au la.

Badala yake, Ikulu imezitaka wizara mbili zilizoibua mkanganyiko huo; Mambo ya Ndani ya Nchi na Afya na Ustawi wa Jamii, kukaa chini na kuondoa utata huo.

Akizungumza kwenye mahojiano na gazeti hili Dar es Salaam  jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, alisema Ikulu haina sababu ya kulizungumzia suala hilo kwa sasa.
“Nataka unielewe, Ikulu hatuna statement (taarifa) ya suala hilo kwa sasa,” alisema Wasira alipotakiwa kuzungumzia utata ulioibuka siku za karibuni baada ya wizara hizo kutofautiana kwa kauli.

Wasira alisema ni mapema mno kwa Ikulu kuingilia mkanganyiko huo, kwa sababu inaamini wizara husika zina nafasi ya kufanya utafiti wa kutosha kuondoa mkanganyiko na kuwapa wananchi taarifa sahihi.

Alienda mbali zaidi akisema waandishi wa habari bado wana nafasi ya kuwaondolea wananchi kiu ya kupata habari za kweli, iwapo watatumia uwezo wao zaidi kwa wizara hizo ili zitoe ukweli badala ya kuibana Ikulu.
“Msitake State House (Ikulu) ianze kulizungumzia suala hilo kwa sasa…  bado nyie waandishi wa habari mna nafasi ya kulifanyia kazi zaidi na kupata ukweli,” alisema.

Dk Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa India kwa matibabu, ambako alikaa takriban miezi miwili na kurejea nchini Desemba mwaka jana.

Ugonjwa unaomsumbua Dk Mwakyembe umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekuwa akishinikia uchunguzi makini kufanyika kwa vile kuna kila dalili za hujuma.

Wasira alisema iwapo waandishi watafanya uchunguzi wa kutosha kupitia wizara hizo wanaweza kupata taarifa sahihi juu ya jambo hilo.Hali hii ilitokana na Mkurugnzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alitoa ripoti akisema uchunguzi wao unaonyesha ugonjwa unaomsumbua Dk Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu.

Siku mbili baadaye, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, aliiruka taarifa ya Manumba akimtaka aeleze alikoipata kwamba hakulishwa sumu.

Wakati Wasira akizitaka wizara kuondoa mkanganyiko huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, ameelezea kuchefuliwa na utata uliopo kwenye ripoti hizo kiasi kwamba hataki kusikia jambo hilo.

“Wala usiniulize kuhusu jambo hilo. Hilo suala wala sitaki kulisikia,” alisema Kombani na katika kuonyesha kuwa suala hilo linamchefua alikata simu alipoona anazidi kumbanwa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+1 #8 2012-02-22 11:54
tonaomba wizara husika kuchukua hatua stahili ili sisi wananchi tujue ukweli ni upi... ajulikane nani anaeleta uongo wa kuliangamizatai fa letu
Quote
 
 
-4 #7 2012-02-22 11:45
Mwakyembe,Mwaky embe,Mwakyembe...all day!Andikeni habari zingine.
Quote
 
 
+1 #6 2012-02-22 10:51
Tusitumie ugonjwa wa Dr. Mwakyembe kujiimarisha kisiasa tufanye kazi kwa uadilifu na kwa mujibu wa sheria
Quote
 
 
+2 #5 2012-02-22 08:38
Selina(kombani) wewe ni waziri mwenye dhamana ya Sheria na Mambo ya Katiba ya Serikali ya Tanzania, hukutakiwa kukata simu au kuchefuliwa na taarifa za Dr Mwakyembe kulishwa sumu, wewe unatakiwa kutueleza kulikoni (wewe ni muhusika mkuu wa jambo hili) kinyume chake utatufanya tuamini ya kwamba wewe ni kati ya wadau wanaochezea afya ya daktari Mwakyembe. Mh Selina kombani usipende kuchafua hali ya hewa kila eneo, kumbuka ulishawahi kuchafua hali ya hewa kwamba hutaruhusu katiba mpya iundwe, matokeo yake imeundwa na bado upo ofisini. Mimi naamini aidha nafasi uliyo nayo huimudu sawasawa au tume huru iundwe mara moja kuchunguza vyeti vyako na mahali uliposomea.
Quote
 
 
+1 #4 2012-02-22 08:31
Kauli ya Wasira ni ya kushangaza kweli! Watoto wako wanagombana kwa mapanga kwa sababu ya ugonjwa tata wa mdogo wao yeye anasema wakae chini watafute ufumbuzi. Kwakuwa Ikulu ndiyo baba alipaswa kusema Ikulu itatafuta ukweli wa jambo hilo kwa kusubiri ripoti ambayo mhusika kasema bado haijatoka ili watanzania wajue kwa uakika kwa suala hilo ili waie na uonga na serikali yao pindi wanapopata maradhi tata wanapotumikia ofisis za serikali
Quote
 
 
+2 #3 2012-02-22 07:46
Kweli sasa nimeamin jambo hili lina mkono wa mafisadi.si wewe tu mama kombani hata mm jambo hili lina ni chefua sana.hata mwakiembe mwenyewe anajiskia vibaya sana sana.
Quote
 
 
+2 #2 2012-02-22 04:56
Tanzania sasa inaelekea gizani. Tunaweza kubishania nani kampa sumu, hatuwezi kubishana juu ya kuwa kinachomsumbua Dk Mwakyembe ni sumu. Ngozi inamwagika, nywele zinanyonyoka na miguu kupasuka ni mwili unatangeza sumu. Hivi tumefikia hapa! Nawaambia mafisadi kuwa, hii si njia ambayo mtu mwenye busara anayoweza kutumia kupambana na anayedhani kuwa ni adui yake! Yumkini kabisa aliyempa Mwakyembe sumu akatangulie yeye na akakosa akiwa hai anachofikiria kukipata kwa kuangamia kwa Mwakyembe.
Quote
 
 
+2 #1 2012-02-22 03:09
Kombani na Makinda wanadhani kuonyesha ukali na kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari wanadhani ndio wataogopwa, au sijui vipi tena. Ni mhimu waelewe kwamba wao ni watumishi tu wa wananchi, na wananchi ndio wanaotaka hizi habari kupitia kwa waandishi wa habari.
Mawaziri wote wanaokataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kwa visingizio visivyo na msingi wanadhani bado wapo kwenye mfumo wa zamani wa kiutawala.
Serikali ni ya wananchi, na habari wanazokataa kuzitoa ni za wananchi.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner