
| Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA | Send to a friend |
| Tuesday, 04 May 2010 23:13 |
|
Emerentiana Masondole na Salim Said “Kama kiongozi wa taifa, rais angetumia maneno ya busara na hekima yasiyo na ukali ndani yake katika kutatua tatizo kwa sababu wafanyakazi wanadai haki yao na wanayo haki ya kufanya hivyo,” alisema Asha alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi majira ya saa 4:30 jana. “Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi.” Bi Asha alikuwa akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, hotuba ambayo iliwashambulia viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wanafiki, wazandiki na wafitini" kwa madai kuwa wamekuwa hawawaelezi wanachama wao kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya pande hizo. Bi Asha, ambaye ni mkulima wa jembe la mkono, alisema rais hakutumia hekima na busara katika kutatua kero za wafanyakazi bali alitumia cheo chake kuwatisha wafanyakazi katika kutetea haki zao. Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa ndio wanaotoa huduma zote muhimu kwa wananchi wote hasa masikini ambao ni wakulima. Alisema rais na familia yake wanatibiwa nje ya nchi ndiyo mana haoni umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi badala yake anatoa majibu ya dharau kuwa kama hawataki kufanya kazi waache. “Au kwa kuwa rais na viongozi wenzake wanatibiwa Ulaya na Marekani ndio maana anatoa vitisho au anataka uwe kama mgomo wa mwaka juzi kwenye Hospitali (ya Taifa) ya Muhimbili ambako watu walipoteza maisha,” alihoji Asha. “Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?” Asha ambaye alitumia muda wa dakika 70 kueleza masikitiko yake, alisema wakati rais anawatisha wafanyakazi ili wasigome, anapaswa kufunga safari kwenda maeneo ya vjijini kujionea hiyo misaada ya matrekta na ‘Power Tiller’ kama imewafikia wananchi au inatumiwa na viongozi wa vijiji kwa maslahi yao. Rais katika hotuba yake alisema serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh315,000 kwa watumishi wa umma kwa sababu wananchi wengine watakosa huduma za afya, pembejeo za kilimo na hata vifaa vya elimu na walimu. “Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi,” alisema Asha kwa hasira. Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Asha alisema enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, bei za vyakula zilikuwa zinafanana katika maduka yote, lakini sasa kila mfanyabiashara ana bei zake. Katika harakati za kutatua tatizo la ugumu wa maisha yake, bibi huyo alisema alishaenda ikulu mara mbili na kugonga hodi ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete ili kuomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara.Asha alisimulia kuwa alifanikiwa kuonana na mmoja wa watendaji wa Wama na kumuelea shida yake, lakini alijibiwa kwamba fedha za Wama zina mlolongo mrefu na kwamba yeye hawezi kuzipata. “Nilipohoji ni mlolongo gani, hakunifafanulia ila aliishia kuniambia tu kwamba ni mkubwa na huwezi kupata fedha hizi... rudi nyumbani. Nikamuuliza je hizo fedha mnazotangaza kwamba mnawakopesha wanawake ni wanawake wote au mna wanawake maalum ambao wanastahiki, sikupata jibu,” alisema Asha huku akionekana kuwa na hasira. Baada ya hapo nilijua kuwa fedha za Wama ni za watu maalum na sio kila mwanamke. “Uongozi ni dhamana aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi: Mungu pia ndiye anayeweza kumnyang’anya dhamana hiyo wala si Watanzania kama anavyodhani, hivyo ajitahidi kuwa mwadilifu, mwenye hekima, busara na imani katika uongozi wake,” alisema Asha.Pia aliwaombea wafanyakazi ambao wanataka kuingia katika mgomo kutofanya hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo watadhulumu haki za Watanzania. “Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin,” alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono. |
| Last Updated on Wednesday, 05 May 2010 22:39 |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Prof Mwandosya aapishwa waziri kazi maalum
- Katiba Mpya: Wananchi Makambako waapa, iwe jua au mvua lazima watoe maoni yao
- Mchakato wa Katiba: Nahodha yupi aaminike? 1
- Wanavyosema wanasiasa kuhusu Katiba mpya
- Serikali inasita nini kutumia Kiswahili kufundishia shule za sekondari?
- Jamii inaweza kuleta mabadiliko katika elimu
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments
Ndg yangu kikwete haongei na wazee wa DAR ANAONGEA NA WANACHAMA WENZAKE,Na pia Jamani wazee wetu mnampigia makofi kikwete lakini jueni mkirudi majumbani sisi vijana wenu ambao tunapigania haki yetu ili kunusuru ugumu wa maisha ulipo ndio tunawalea kwa kula yenu kuvaa mpaka matibabu yenu sijui kwanini manashindwa kumbana pindi akiwaita?
Tunajua wewe unaomlaumu mnyika ni nambari wani kwa hatujui umemuona mnyika yupo juu unaleta fitina mbona wewe ukugombea ubunge na ukigombea hata mwenyewe utajisahau kujipia kwamaana utapa sifuri
Hili ni gazeti la wananchi tuache tutoe maoni yetu kama uwezi wewe soma magazeti ya Habari leo, Uhuru na mzalendo.Maana magazeti hayo ukitoa maoni umetukana serikali hata ujumbe wako uoni kabisa.Big up mwananchi kwa kujali wananchi na maoni yao
If your guess is right, take my kudos and be happy brother Tesha. But because I am not a member of Chadema political party, your prognosis is simply another Yahya’s false prophecy...full of unrealistic guesses. Just keep on with your fallacies as your wish.
And U too! U're hired and paid filthy money by CHADEMA