MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Lowassa apata kikombe Loliondo
BOOKMARK THIS PAGE
Lowassa apata kikombe Loliondo  Send to a friend
Tuesday, 15 March 2011 23:47

Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.

Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.

Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”

Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini ambao wameshafika kwa mchungaji huyo kupata tiba hiyo wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya.


Katika jitihada za kudhibiti usalama na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma kwa mchungaji huyo bila matatizo, Serikali imeimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), katika kijiji hicho na kusimamia magari. Pia imepeleka wauguzi kusaidia wagonjwa mahututi kabla ya kumfikia mchungaji na imetoa pia jenereta kwa ajili ya kufua umemeKaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymond Mushi alisema jana kuwa, sasa walau hali ni nzuri kwani msongamano umepungua.


"Ni kweli sasa hali inaridhisha na jana watu wamekwenda kupata tiba na kurejea makwao mapema hili ndilo serikali inalolitaka. Tunaomba watu wanaopeleka wagonjwa wawe wanauliza kwanza hali ya msongamano," alisema Mushi.Mushi alisema inawezekana watu wanaokwenda katika kijiji hicho kusubiriana katika Mji wa Mto wa Mbu ambako kuna huduma nyingi muhimu kuliko wote kwenda huko kwa wakati mmoja.

Alitoa wito kwa watu wenye wagonjwa mahututi kuacha kuwapeleka moja kwa moja kwa mchungaji huyo kabla ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao.Katika hatua nyingine, wagonjwa kadhaa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wameanza kutoroka wodini na kwenda Loliondo kupata matibabu ya magonjwa sugu yanayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile, Mwananchi imeelezwa.

Habari zilizopatikana hospitalini hapo jana zimeeleza kuwa wagonjwa hao walianza kuondoka Muhimbili juma lililopita baada ya Serikali kubariki matibabu hayo. Ofisa mmoja mwandamizi wa hospitali hiyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, amesema kuwa wakati baadhi ya wagonjwa hao wakiwa wanatoroka wodini, wengine wamekuwa jasiri kwa kuwaaga madaktari wao.

“Wagonjwa wameanza kuondoka na wengine bila hata ya kuaga, hivyo hatujui hatima yao kama watafika salama huko Loliondo,” alisema.Ofisa huyo alisema juma lililopita, mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa chumba namba 15 katika Wodi ya Kibasila, aliondoka baada ya kusikia taarifa kuhusu huduma hiyo.

“Kuna mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa Kibasila Wodi namba 15 aliondoka aliposikia kuwa Babu ameanza tena kutoa matibabu hayo ambayo awali yalisitishwa,” alisema.Hata hivyo, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaisha alisema hana taarifa za kutoroka wodini kwa wagonjwa hao na kwenda kufuata tiba huko Loliondo... “Sina taarifa zozote za kuondoka kwa wagonjwa hapa hospitalini.”

Matibabu Loliondo yapandisha nauli Ubungo
NAULI za kwenda Arusha kutoka Ubungo, Dar es Salaam zimepanda kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na wingi wa wasafiri wanaoelekea Loliondo kupata tiba hiyo ya magonjwa sugu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka kituoni hapo zimeeleza kuwa, nauli hizo zimepanda kutoka Sh18,000 hadi Sh30,000 tangu juma lililopita.

Mmoja wa mawakala wa mabasi ya abiria katika kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ongezeko hilo la nauli limetokana na baadhi ya mawakala kukodi mabasi na kuwasafirisha abiria.“Nikupe siri moja tu ambayo inatufanya tupandishe nauli. Lengo letu ni kupata faida, ujue sisi tunakodi basi zima kisha tunakatisha tiketi kwa bei yetu ili na sisi tupate faida,” alisema.

Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Arusha, Charles Manyama alisema mabasi yaendayo huko yamegawanyika katika madaraja matatu yale ya bei ya juu, bei ya kati na bei ya chini lakini kwa sasa bei imekuwa ni moja kwa mabasi yote.

Kwa mujibu wa abiria huyo, zamani nauli za Arusha zilikuwa Sh25,000 kwa basi la daraja la juu, Sh18,000 kwa mabasi ya daraja la kati na Sh15,000 kwa daraja la chini, lakini sasa mabasi yote yanatoza kati ya Sh25,000 hadi Sh30,000.“Mawakala hawa wanadhani kila mtu anayepanda magari haya anakwenda Loliondo lakini siyo kweli, wengine tuna safari nyingine kabisa," alisema Manyama na kuongeza:

"Unakuta bei zinashangaza na kupanda sana. Hata hivyo, inashangaza kuona wanadamu tunakosa utu. Watu wanakwenda kupata matibabu wanapandishiwa nauli, walipaswa kuwaonea huruma wagonjwa hawa,” alisema Manyama.Jitihada za kumtafuta Meneja wa kituo cha mabasi Ubungo ziligonga mwamba baada ya taarifa kutoka ofisi kwake kueleza kuwa alikuwa nje kikazi.

Polisi Arusha wadhibiti usafiri wa Loliondo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha kuweka vituo vinavyotambulika kwa ajili ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu kwa Mchungaji Mwasapile ili kuepuka utapeli.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu kutaka kwenda Loliondo, kumezuka vituo vingi ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha utapeli kwa watu wanaotoka mikoani."Nafahamu hili ni jambo ambalo manispaa wanahusika nalo, wahakikishe kuwa hakuna vituo visivyo rasmi ili wananchi wasije kudanganywa na watu wabaya," alisema.

Katika kituo kilichoibuka ghafla baada tiba ya magonjwa sugu kuanza kutolewa cha Chini ya Mti, kulizuka vurugu za madereva na madalali waliokuwa wakibishania kiwango cha nauli, hatua iliyosababisha polisi wenye silaha kupelekwa katika eneo hilo.

Hatua ya polisi kuonekana katika kituo hicho, ilisababisha wasiwasi kwa wananchi kuwa huenda Serikali imesimamisha utaratibu wa wananchi kwenda Loliondo, jambo ambalo kaimu kamanda huyo alilikanusha.

"Tunachokifanya ni kuweka utaratibu mzuri, polisi wanasimamia sheria. Magari mengine yanazidisha idadi ya watu na kutoza pesa nyingi zaidi. Sumatra wakisema nauli sahihi ni kiwango fulani na madereva wakizidisha basi tunawakamata," alisema.

Wananchi waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao walisema kuwa wanashangazwa na bei ya nauli kuwa juu hata baada ya Serikali na KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati kuboresha mazingira ya kuwahi kupata tiba na kuondoka kijijini Samunge.

"Mwanzoni walikuwa wanasema magari yanakaa sana huko, kwa hiyo wanafidia hizo siku za kungoja wagonjwa lakini sasa hivi ukienda leo unarudi kesho na nauli bado iko juu," alisema mmoja wa wananchi hao.Nauli ya kutoka Mjini Arusha hadi Samunge, Loliondo ni Sh100,000 kwenda na kurudi kwa magari aina ya Land Cruser ,huku nauli ya mabasi ikiwa pungufu zaidi.

Habari hii imeandaliwa na Nevile Meena, Ibrahim Yamola, Dotto Kahindi Dar na Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Arusha


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 17 March 2011 07:39
 

Comments 

 
0 #56 2011-05-25 10:13
kwa bahati nzuri wanaosoma maoni wengi tunategema wameona mbali,kwa maana ya kwamba kuweza kutumia mtandao.sasa basi ni vizuri tuelekeze maoni yetu kwenye vitu ambavyo vitasaidia wasomaji kupata ukweli wa mtatizo yetu Watanzania,nini tunahitaji, wapi tunapata ufumbuzi,nani wa kutatua swala hilo,basi ikiwa unajua toa maelezo yalio nyooka ili iwe rahisi kwa wahusika kunyookea pale kwenye tatizo.Mtu anayesema yasiofaa au yanyokera tusimjibu ili abaki na yake yasiofaa kichwani mwake,tuendelee kuelisha wanaopenda maendeleo na kuwajulisha nini wanatakiwa kufanya ili kulinusuru Taifa letu. Na ushauri wangu kwa viongozi wa dini ni vyema kutaja maovu lakini ni vyema zaidi kufanya mafungo maalumu kwa viongozi hawa ili Mungu afanye maamuzi kwani yeye ni mwisho wa yote na tukimtegemea yeye tutapata majibu wala si kwa nguvu zetu,AMENI.
Quote
 
 
0 #55 2011-05-25 09:39
Ni vyema tukawa watekelezaji kwa vitendo kwa sababu hawa vijana wanaoingia sasa wataiga mfano gani endapo waliotangulia ni lazima ipite kauli maalumu ndipo jambo litendeke,mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.Sasa mnalingia usomi gani kama kila kitu lazima iundwe Tume,kama hujui wajibu wako wewe si msomi wala elimu yako haina maana kwa jamii.hapa tunacho hitaji ni kila mmoja kupitia taaluma aliosomea kutekeleza mambo muhimu pasipo magazeti wala wanasiasa kuingilia kati ni aibu.Asie na elimu asimamiwe na wewe mwenye elimu usimamiwe je tofauti yenu ni nini
Quote
 
 
0 #54 2011-03-17 05:56
Lowasa Rais wetu wa 2015. anatufaa. dawa ya babu itampa nguvu. acheni chuki za ki[NENO BAYA] ki[NENO BAYA]. hivi leo babu akisema ameoteshwa na Mungu kuwa Lowassa ndie anaefaa kua Rais mtampinga?
Quote
 
 
0 #53 2011-03-17 04:10
na nyie gazeti la mwananchi ni WA PU MBA VU KABISAAAAAAA MMEKOSA HABARI ZA KUANDIKA,KILA SIKU HABARI ZA BABU TU,SASA NA GAZETI LA UWAZI WAANDIKE NINI!!!!!!!!!!!
Quote
 
 
0 #52 2011-03-17 04:08
paul,ni kweli kabisa,manake kuna watu wasipoandika kuhusu mapadri hawajisikii kabisaa,tatizo hawakuelewa na kusoma vizuri mahubiri ya Pengo.
Quote
 
 
0 #51 2011-03-17 04:04
Quoting SLAA:
TATIZO LA HAWA MAASKOFU NA MAPADRI SIKU HIZI DINI IMEKUWA BIASHARA YANI KANISA LIMEKUWA KIMBILIO LA WATU WANAOTAFUTA UTAJIRI AMA PROTECTION YA MAISHA NA SIO KWAMBA NI WACHAMUNGU WA KWELI NA NDIYO MAANA KAULI ZAO NYINGI SIKU HIZI ZIMEJAA SIASA KULIKO UHALISIA WA MAMBO.

HAPA SASA KANISA LIMESHAKUA DILI LA KUJIPATIA AMA KUTIMIZA MATAKWA YA WATU WACHACHE NA NDIYO MAANA SIJASHANGAA KUSIKIA KAULI ZA KAKOBE AKIMPONDA NA KUMTOLEA MANENO MACHAFU NA YAVITISHO BABU LOLIONDO NA HUYU NAE PIA UTAKUJA KUMSIKIA MUDA SI MREFU MAMA RWAKATARE NAE AKITOA KAULI KUMPONDA BABU KUTOKANA ANAHATARISHA BIASHARA ZAO NAO LAZIMA WAFANYE MARKETING.
WANAMSANIFU BABU KUWATOZA WATU SHILINGI 500 WKT WAO WANATOZA WAUMINI KILA KUKICHA MAELFU AU MALAKI YA SHILINGI KWA KIVULI CHA JINA LA SADAKA KAMA HUTAKI KUTOA BASI UNATENGWA NA KANISA NA HAWATOSHIRIKI CHOCHOTE KUHUSIANA NAWEWE,WANATUMI A MICHANGO YA WAUMINI KUTEMBELEA MAGARI YA KIFAHARI,MAJUMB A YA KIFAHARI NA KUISHI MAISHA YA ANASA.

PIA SIWEZI KUSHANGAA KWA KAULI ZILIZOTOLEWA NA ASKOFU MKUU KATOLIKI KUSHAMBULIA SERIKALI YA KIKWETE NA KUDIFENDI CHADEMA KUTOA KAULI ZA KICHOCHEZI KUIGAWA JAMII HII INATOKANA NA KUWA SERIKALI YA KIKWETE NI SERIKALI AMBAYO IMEBANA NA KUHATARISHA MASLAHI YAO AMEBANA BISHARA ZAO HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA,KUUZA PEMBE ZA NDOVU NA FARU SIKU HIZI MAGARI YAO YANAKAGULIWA SIO KAMA ZAMANI PIA ALIFUTA MSAMAHA WA KODI KWA TAASISI ZA KIDINI,HAWA NI WATU HATARI SANA WASIOJARI MASLAHI YA TAIFA LETU RWANDA NA BURUNDI WALICHANGIA SANA MAUAJI YA HALAIKI.
TUJIFUNZE WATANZANIA NA KUWA MFANO WA KUIGWA KAMA KANISA LA ANGLICANA.
NAJUA WAPO WASHABIKI NA MAMLUKI WATAKAOCHUKIA UKWELI NILIONGEA HII KUTOKANA NDIVYO WALIVYOFUNDISHW A NA VIONGOZI WAO KAMA HAO WANAOJIITA MITUME ILIKULINDA MASLAHI YAO BINAFSI


we ngedere jiheshimu kabisaaaaaa,ten a uchunge huo ulimiwako mkali kama wa ndege,soma vizuri mahubiri aliyoota Pengo,alisema KAMA MAANDAMANO YA CHADEMA BAADA YA UCHUNGUZI YAKIONEKANA YANAWEZA KULETA MADHARA BASI YADHIBITIWE,sas a unataka kusema anamtetea Slaa hapo? pu mba vu kabisa wewe soma vizuri uelewe habari na sio kupapatikia tu kama kinda la bundi!! halafu hakuna Padri aliyepinga huduma ya Babu,pia,Pengo ameonesha wasiwasi tu kuhusu hiyo huduma,hajasema haina ukweli,we ngedere jiheshimu na usome kwa kuelewa usirukie rukie tu.
Quote
 
 
+1 #50 2011-03-17 01:07
NDIO KAENDA!! SO WHAT?
MMEKOSA MAMBO MUHIMU YA KUANDIKA JAMANI? MAGAZETI YA UDAKU YAANDIKE NINI SASA KAMA MNAANDIKA MAMBO YASIYO NA MANUFAA YEYOTE KWA JAMII,,JAMANI TUNAMAMBO MENGI YA KUANDIKA KAMA HUU UKURASA HAUNA CHA KUANDIKA NAOMBENI MNIPE MIMI KAZI NIWAPE MAMBO YA MSINGI MUANDIKE...
Quote
 
 
0 #49 2011-03-16 23:10
Wote mmeonge na nimesikia kama mimi mtanzania,lakin i nachotaka kwenu kuongea hakutoshi wala kutoa mchango kama huu,nachotaka kusikia, Tanzania inapona kutoka mikononi mwa watu wenye nia mbaya kwa kuiangamiza,Ina pona kwa kuomba Mungu na si kama watanzania tulivyo watu wa kuongea sana,Mungu yupo na tukimuomba anasikia, amesema hamna kitu kwa sababu hamuombi,chakuf anya sasa watanzania tuombe,la sivyo tanzanaia baada ya miaka mitano basi;
Quote
 
 
0 #48 2011-03-16 22:23
Yaan mnasema Lowassa awe Raisi 2015 mmefilisika mawazo kabisa alivyochafuka kisiasa nani atataka tena kumpa rungu nyie mpe rungu ila baadaye msilaumu pindi mkipata manundu Mwalimu alishasema kuwa anatufaa kunywa nae chai na wiski ila sio uongozi nadhani watanzania wanahitaji fimbo huwez kutoa michango kama hii ukiwa kweli na akili zako
Quote
 
 
-2 #47 2011-03-16 21:59
Kwa mtu mwenye akili timamu anajua kuwa Mtu anayefaa kuwa Rais 2015 ni Edwald Lowassa. Huyu ndiye Rais wa Tanzania 2015. Hakuna mpinzani.
Quote
 
 
-2 #46 2011-03-16 20:10
Mambo mswano,Edward poa sana tunakua wewe ndiye rais anaweza kusu[NENO BAYA] gurudumu la taifa letu mbele,sasa hivi huku kwetu Temeke kila nyumba watu wanakwenda sekondari,tunak ungoja uje kujenga maabara kwa maana ile speed haipo kabisa.
Quote
 
 
0 #45 2011-03-16 18:44
babu tafadhali, weka kitabu cha wageni..
tunataka kuona waliofika, wenye afya mbofumbofu na wenye kijifanya wazima kumbe wabovu,na zaidi kuweka kumbukumbu...tena ikiwezekana uwe unatwanga na picha kabisa.la mwisho, wapige mkwara, wasipotengeneza barabara na kuweka taa njiani na ikiwezekana lami..basi unasitisha zoezi zima na kila kiongozi aliyekunywa dawa ,ambae kwa namna moja au nyingine anazorotesha maendeleo ya nchi, ile dawa haitafanya kazi ,na itakuwa sumu mwilini na unatoa simu 30 tu.
Quote
 
 
0 #44 2011-03-16 18:27
IMANI NIKUWA NA HAKIKA NA MAMBO YATARAJIAYO NI BAYANA NAYASIYO ONEKANA.HAO WACHAMUNGU WANGEENDELEA KUOMBA KWA AJILI YA HILO BILA KUKASHIFU.UNAWEZA UKAKUTA MUNGU AMEAMUA KUJIINUA KWA NJIA HIO BAADA YA KUONA WANAOLITAJATAJA JINA LAKE,WANAMAPUNG UFU.MUNGU KAOTESHA MTI OMBEA NINYI VIONGOZI WA DINI.MUJIBIWE NA MUNGU ALIYE HAI KAMA NIYEYE KATOA HIYO DAWA?BALI ACHENI KUKASHIFU MAANA WATU WALIO KATA TAMAA WATAWADHARAU
Quote
 
 
0 #43 2011-03-16 18:03
Quoting Kalunde:
Mwananchi asanteni sana kwa umakini wa kutoa taarifa nyeti kwa jamii ya kitanzania. Hongereni sana. Lakini pia niungane na Muheshimiwa Lowasa kuwaambia kwamba habari za viongozi kwenda Loliondo si NEWS kwa kweli. Si wameenda tu, kwani baada ya hapo wao wakienda sisi tunafaidika nini? Hebu tuache udaku jamani, tusiwe kama haya magazeti mengine, turudi kwenye mambo ya tija yanayohusu mstakabali wa taifa letu. Tuelezeni utumbo unaofanywa na serikali yetu ili tupate kujua. Mambo mengi tu kwa kweli.

Serikali inafurahia sana sasa inapoona kuna shift toka kuzungumza na kuweka maovu yao hadharani na sasa attention yote iko kwa babu. Tusiwaachie, endeleeeni kuwasakama na kuanika uovu wao kwa nguvu zaidi, ari zaidi kwa masiha bora ya watanzania.

Aluta Continua

Kalunde

lowasa saiv ni mwema?
Quote
 
 
-3 #42 2011-03-16 17:33
babu anatisha ila inabidi awe na kitabu kinacho onyesha mchanganyiko wa tiba kwa ajili ya kizazi kijacho
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner