
| Mtaalamu asisitiza mafuta yamepatikana | Send to a friend |
| Saturday, 19 June 2010 21:28 |
|
Mwandishi Wetu MTAALAAMU wa kimataifa wa nishati amesema, upatikanaji wa mafuta nchini Tanzania umefikia katika hatua za kuridhisha. Katika mahojiano na gazeti hili jana, Dk Philip Nelson, alisema mafuta na gesi sasa yanapatikana katika mfumo mpya wa kutumia bahari. Alisema Februari 2008, Kampuni za Petrodel Resources Limited (PRL) na Heritage Oil Limited, kwa pamoja walifanya uchunguzi katika bahari, magharibi ya Visiwa vya Mafia. “Nilikuwa na uhakika kuwa naona DHIs katika taarifa zilizohifadhiwa TPDC, hivyo kwa msaada wao, tuliweza kutengeneza karatasi safi tulizozichapisha kutoka katika filamu ya TPDC. Baada ya hapo, tukabadilisha picha kwa mfumo wa kitaalamu na kuzihamisha taarifa hizo kwa kompyuta maalumu ili kupata picha nzuri zaidi," alisema Dk Nelson. Hata hivyo, alisema mbali ya hapa Tanzania alifanya kazi ya utafiti kwa miaka mitatu nchini Nigeria akifanya katika kampuni ya mafuta ya Petroleum Development. Alisema kuwa maeneo yenye visima hivyo yanapatikana huko Latham, Kimbiji. Mtafiti huyo alisema visima vimefikia urefu wa mita 3,500 baada ya kuchimba mzunguko ambao ni sawa na asilimia 90. “Visima vimefikia urefu wa kiasi cha meta 3,500, baada ya kuchimba kwa mzunguko sawa wa asilimia 90, hali ni nzuri kwa mabwawa ya miamba kwa ajili ya kukusanya mafuta, lakini hakuna kifungo cha kuzuia mafuta yatakayopita katika mzunguko huo” alisema Dk Nelson. Alisema, Petrodel imedhamiria kutafuta na kuzalisha mafuta na gesi kwa manufaa ya Watanzania. ‘Tanzania, ni nchi nzuri yenye watu wazuri na wakarimu, nina bahati kubwa kukutana nanyi ni sehemu nzuri kufanya kazi na Rais ametengeneza mazingira yanayowezesha biashara bora,” alisema Dk Nelson. Mtaalamu huyo aliongeza kuwa,Desemba 2008, kampuni ilipata eneo la kilometa 1,200, za mafuta katika bahari na kwamba taarifa hizo zimeonyesha hali ya kuridhisha ya upatikanaji wa mafuta na gesi. Dk Nelson ni mtafiti wa mafuta mwenye ujuzi wa karibu miaka 45 katika sekta za viwanda na gesi. Vilevile alifanya kazi hiyo katika kampuni ya utafiti wa mafuta nchini Uingereza kwa miaka 6. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Prof Mwandosya aapishwa waziri kazi maalum
- Katiba Mpya: Wananchi Makambako waapa, iwe jua au mvua lazima watoe maoni yao
- Mchakato wa Katiba: Nahodha yupi aaminike? 1
- Wanavyosema wanasiasa kuhusu Katiba mpya
- Serikali inasita nini kutumia Kiswahili kufundishia shule za sekondari?
- Jamii inaweza kuleta mabadiliko katika elimu
- Nafasi za Kazi
- Links za wateja na washirika wetu
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani















Comments
sidhani kama ni magharibi mwa visiwa vya mafia bali ndani ya visiwa vya zanzibar kwa hiyo hakuna mwisho mwema kwa maana wazanzibar hawataki mafuta yawe ya muungano
Kwa madini na raslimali nyingine nyingi tulizo nazo, tungekuwa na watawala wanaotumia common sense tu, tungekuwa kama Botswana. Utajiri bado utapatikana na wahindi watauhamishia India.
Sasa sakata liko kwa viongozi wa nchi yetu.
Je,wananchi watanufaika kwa jinsi yoyote ile katika hatua hii ya kuwa na visma vyetu wenyewe?Hadi sasa tuna visima vya kutosha vywa gasi tukitegemea kushuka kwa kiwango cha mwananchi wa kawaida kumudu kutumia gasi badala ya kuni na kunsuru janga la jangwa nchini;lakini bado matumizi ya gasi kwa mwanach wa kawaida ni njozi.nchi jirani zatumia gasi yetu kwa bei nafuu kuliko TANZANIA.Tunaomba miujiza kutoka kwenu ,Waswahili hema,Mcheza kwao hutunzwa.NCHI NYINGI ZENYE UWEZO NI ZILE ZINAZOWAJALI WANANCHI WAKE KWA KUHAKIKISHA KILE KINACHOPATIKANA NCHINI KINABAKI NCHINI.HATA HAO WANAOTULETEA MISAADA HULETA WATU WAO NCHINI NA WAWAAJIRI KWA PESA HIZOP ZA MISAADA wanazotudangany a nazo.mimi.....sijui
mdau
Moro.
Had