MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari Chadema, CCM, CUF zakabana koo Z'bar
BOOKMARK THIS PAGE
Chadema, CCM, CUF zakabana koo Z'bar  Send to a friend
Sunday, 05 February 2012 10:13

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
VYAMA vya siasa vitatu, Chama cha  Demokrasia na Mandeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinachuana vilivyo uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini, visiwani hapa.

Uchunguzi uliofanywa wiki moja tangu kipenga cha uchaguzi huo kipulizwe, vyama hivyo vitatu vimeonyesha kung'aa kutokana na kusambaza mabango na bendera karibu kila kona ya jimbo hilo, huku vikiwa ni gumzo kwenye maskani mbalimbali.

Hii inaashiria Chadema safari hii wamejidhatiti katika siasa za Zanzibar ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikitawaliwa na vyama viwili, CCM na CUF.
 
Chadema kwenye uchaguzi kimemsimamisha Maalim Ali Mbarouk Mshimba, kuwania kiti hicho, CCM, Mohamed Raza na CUF Salma Hussein Zarali.

Mambo yanayoashiria Chadema kwa mara ya kwanza kuingia na nguvu kubwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar ni kusikika kwenye magumzo ya vijiwe sawia na CCM na CUF.

Tayari Chadema kimeaanza kulia kufanyiwa rafu baada ya watu wasiojulikana kusambaza waraka unaodai kuwa Maaskofu Tanzania Bara wanakibeba chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Hamad Yusuf Musa amkiri kupata taarifa za kusambazwa kwa waraka huo lakini akauelezea kuwa ni propaganda chafu dhidi ya chama hicho baada ya kuonekana kuwa na nguvu jimboni humo.
CUF kwa upande wake, kimeanza kampeni hizo kwa kishindo huku kikitumia uzoefu wake wa siasa za Zanzibar kutaka kuibuka mshindi.


Kwa upande wa CCM, chama hicho kimeendelea kujidhatiti kwa kampeni za wazi na vikao vya ndani katika kuhakikisha mgombea wao, wananyakua kiti hicho ambacho kilikuwa kikishikiliwa na Mbunge Mussa Khamis Silima aliyefariki dunia Agosti mwaka huu.

Mgombea wao, Raza ambaye ni mwanasiasa na kada wa muda mrefu wa chama hicho, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini mojawapo ikiwa ni ya mshauri waa Rais Mstaafu, Salmin Amour, kuhusu mambo ya michezo.

Vyama vingine ambavyo navyo vinajiwinda katika kuwania kiti hicho ni TADEA ambao wamemteua, Khamis Vuai Haji kuwa mgombea wao na AFP, Rashid Yusuf Mchenga.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2012-02-10 08:20
siasa visiwani zinaelekea kukomaa na kupevuka,wahafi dhina waache kuleta siasa za kibaguzi,zitawa geuka!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner