MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne
BOOKMARK THIS PAGE
Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne  Send to a friend
Saturday, 15 May 2010 22:14

ASEMA WAKATI  WAKE RUSHWA HAIKUWEPO
Hadija Jumanne
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, mzee Ali Hassani Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa ameshangaa kukithiri kwa rushwa katika utawala wa awamu ya nne ikilinganishwa na tawala zote zilizopita.


Mzee Ruksa alisema hayo jana jijini Dar e Salaam katika mahafali ya 12 ya Chuo cha Teknologia ya Habari (IIT) alikoalikwa kama mgeni rasmi.
Alisema kuwa miongo miwili iliyopita, akiwa madarakani kama rais wa awamu ya pili rushwa ilikuwa haipo na ilikuwa haina nafasi.

Mwinyi alibainisha kwamba, wakati anatangaza ruksa kwa kila kitu hapakuwa na rushwa wala mianya yake.


“Kipindi mimi niko madarakani miongo miwili iliyopita, rushwa ilikuwa haipo na hata wakati natangaza kila kitu ruksa katika serikali yangu, kulikuwa hakuna mifuko ya rushwa serikalini wala katika sekta binafsi,” alisema Mwinyi.

Alisema anashangaa kuona rushwa inakithiri katika serikali ya awamu ya nne (ya rais Jakaya Kikwete) huku mianya yake ikizidi kuongezeka kwenye taasisi za umma na sekta binafsi.

“Inashangaza kuona rushwa imeota mizizi katika sekta mbali mbali hapa nchini kitu ambacho kinakwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi,”alieleza Mwinyi.

Rais huyo mstaafu aliwataka vijana waliohitimu katika chuo hicho wakatumie ujuzi walioupata kujiajiri na siyo kusubiri kuajiriwa au kupata nafasi serikalini.

Aliwataka pia kuwa wapambanaji wa rushwa ambayo imeota mizizi katika sekta mbalimbali nchini.

Alipoingia madarakani miaka mitano, iliyopita Rais Kikwete aliahidi kuwa serikali yake itaongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa na kwamba, atafanya hivyo kisayansi kwa kushambulia kiini chake.

“Kwa kadri mapato ya Serikali yanavyoongezeka, ndivyo tutakavyoongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Jeshi la Polisi na mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo," alisema Kikwete.

Kikwete alisema hayo Desemba 30, 2005 wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania na kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwenye mapambano hayo.

"Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi,” alisema Kikwete na kuongeza kuwa mbali ya hayo, alibainisha kuwa katika kupambana na rushwa ataangalia kwa ukaribu suala la mikataba.

Alieleza kuwa serikali yake inakusudia kuangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa, hasa zile kubwa. Hata hivyo, katika juhudi za serikali ya awamu ya nne kupambana na rushwa, kesi mbalimbali za rushwa kubwa zinazofikia 25 zipo mahakamani.

Aidha, mwaka huu serikali imerekebisha sheria na kuipa meno Takukuru ili kuipa nguvu zaidi ya kupambana na tatizo hilo, na kidhinisha sheria mpya ya gharama za uchaguzi inayolenga kudhibiti na matumizi ya fedha haramu katika uchaguzi.

Katika mahafali hayo, Mwinyi alitoa shahada ya kwanza, stashahada na stashahada na digrii kwa wahitimu 150 katika masomo ya teknolojia ya habari, biashara na kompyuta.

Wahitimu 15 kati ya 150 ambao walichukua shahada ya teknologia ya habari walitunukiwa tunzo maalum baada ya kufanya vizuri katika masomo hayo.

Wahitimu wengine 50 pia walitunukiwa tuzo katika masomo stashahada na wengine 85 stashahada ya kompyuta na biashara.

Chuo hicho kilianzishwa Mei 1990 chini ya jina Microtek Computers Limited kabla ya kubadilishwa mwaka 1992 na kuwa Taasisi ya Teknologia ya Habari(IIT).
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Mujtaba Salemwalla, alisema kuwa elimu hiyo waliyopewa vijana hao hawana budi kuitumia ipaswavyo kwani wamebeba jukumu la kuihudumia jamii.
Chuo hicho kwa sasa kina matawi mawili katika jiji la Dar es Salaam, katika jengo la Kelvin lililopo mtaa wa Samora na katika jengo la Africab Tower barabara  ya Kawawa  karibu na Machinga Complex na kinatoa shahada na stashahada.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #16 2011-08-16 13:47
usiache mbachao kwa msala upitao ndio tatizo kubwa kwa vioongozi wetu kwani wanaogopa kusema ukweli halisi .

haya na wengine semeni...lakini muanze kusema ya kwenu kabla hamjasema ya wenzenu
Quote
 
 
+2 #15 2010-10-15 18:00
Mwinyi uko sahihi.Ee Mungu uturehemu, kizazi hiki kinachoita 2 billion "VIJISENT" kinachotumia mabilioni katika kampeni. kinachoomba rushwa kwa mgonjwa aliyoke taabani.
Quote
 
 
+3 #14 2010-05-22 12:17
na watanzania tunafanya nini kuwaengua viongozi kama hawa au tunaongea vizuri hapa halafu kwenye uchaguzi tunawapa kura zote na mwendo unakuwa wa kasi zaidi.
Quote
 
 
+2 #13 2010-05-19 13:28
Wananchi waisaidie serikali kupambana na vita vya rushwa na hilo liloibuka miaka ya hivikaribuni ufisadi siyo kauli kigeni kwetu, tunachoshindwa kufahamu ni hivi, baada ya wito kama huo kwa miaka mingi bila mafanikio serikali ina mbinu zingine zipi? Ni dhahiri kwamba mbinu hiyo ya wananchi kutoa taarifa inaonekana ni dhana dhaifu, je serikali inamikakati gani mingine ya kukabiliana na matatizo hayo mawili vinavyozidi kusitawi na kutanda kama mikongo ya viazi ninavyostawi wakati wa mvua, ambapo ni dhahili vinapunguza kasi ya vita vya kumkomboa mnyonge.
Kikawaida hakuna tatizo lisilotatulika, ni ukosefu wa WITO na DHAMIRA YA DHATI. Tunafahamu wazi serikali wanafahamu vizuri sana kitu cha kufanya kama wataamua kuviangamiza rushwa + ufisadi. Tatizo mbinu hizo ni kugeuka kuwa mtego wa panya kwa waliopo na wasiokuwemo, pengine hata kukumba baadhi ya wategaji. Mtokeo yake ni kutumia mbinu zozote zitakazoweza kuonyesha serikali inayashughuliki a ili kutuliza mioyo yao.
Quote
 
 
+1 #12 2010-05-19 11:46
Mzee Ruhsa, rushwa ilikuwepo hata wakati wako kama kawaida. Labda tofauti ni kwenye kiwango (the degree and level of corruption) lakini siyo kuwepo kwao. Lakini pia kipindi cha awamu ya kwanza na ya pili hakukuwa na uhuru wa habari kama ilivyo sasa. Hivyo matukio ya rushwa yalikuwa vigumu hata kuandikwa na kuripo[NENO BAYA].
Quote
 
 
+3 #11 2010-05-19 11:28
Ati serikali inaomba wananchi wasaisaidie kukabiriana na rushwa, 1.kuna swala la watu kuhofia maisha yao 2.mtu kudharauliwa atakapotoa taarifa (vithibitisho kibao vitahitajika) 3.mlolongo wa kumfikia mtu atayeshughuliki a swala, kama maneno yangelikuwa yanavunja mfupa tusingelihitaji shoka, mapanga wala visu kwenye mabucha wala majumbani. Serikali imezungumzia swala la ukomeshaji wa rushwa + ufisadi, kadiri inavyojaribu kukemea maswala hayo ni kama vile mtu umemwaga petrol kwenye moto.
Serikali ina mapanga, mashoka na visu vyake amavyo ni sheria na vyombo vya usalama wa taifa, je matumizi ya vyombo hivi ni kwa ajili ya wachache wanaodhaniwa kuwa maisha yao yanaweza kuwa hatarini kutokana na kazi zao au wajibu wao tu? Au pia wajibu kwa ajili ya ustawi wa kila raia wa tanzania? Kwa hiyo swala hapa ni ukosefu wa dhamira ya dhati ya kutokomeza tatizo hilo. Mika nenda rudi wananchi wameombwa kuisaidia serikali kuhusiana na matatzo hayo, baada ya kutoona matunda Serikali inamipango gani?
Quote
 
 
+2 #10 2010-05-18 04:07
Aibu kwa mwandishi kipande kilichoingia para ya 11 -14 cha rais kikwete kiko kw qjili ya kumtetea rais sijui ni mhariri wakati anahariri ndio kakiweka au mwandishi kaamua kwani hakina maudhuwi ingeeleweka kama angelinganisha para hizo na rushwa katika kipindi cha sasa,kuhusu mzee mwinyi anaongez chumvi kwa kudai rushwa hikuwapo katika wamu yake si kweli ila haikuwa kubwa kama sasa kulikuwa na hofu kwani mwalimu nyerere alikuwa hai, hata mkapa alianza rushwa baada ya kifo cha mwalimu. ni mtazamo batili na kauli isiyoongozwa na ukweli kwa mzee ruksa kudai hivyo.mifano michache ya rushwa katika awamu ya mwinyi ni pamoja na mwananwe hassan kuhusika ktk wizi wa madeni ya nje DCP (debt conversation program),nimrod mkono na v.g.chavda hayo ni machache tu. ni vyema kama kiongozi wa zamani akatoa kauli ya kujutia utawala wake na kuonya utawala uliopo kwa rushwa na sio kudai kinyume.
Quote
 
 
-4 #9 2010-05-17 21:06
JAMANI MDOMO NI MALI YAKE MWACHENI AMSEME MWANACHAMA MWENZIE ILI WAJUE TULIKOTOKA ,TULIPO, NATUENDAKO HAJUI NI MWANAMKE WA NANI ALINUNUA NDEGE YA ABIRILIA? BASI LABDA ANGESEMA MIMI NA JK NANI ZAIDI KWA RUSHWA?
Quote
 
 
-3 #8 2010-05-17 17:58
Mzee Mwinyi tunakuheshimu sana wewe sasa
kwenye siasa basi au nimtume tena kijana mwingine akuzabe kofi.Umepumzika kuwa mtawala wa nchi hii usitukumbushe machungu ya Loliondo uliyotuachia.
Quote
 
 
+2 #7 2010-05-17 13:49
Kusema kweli political system yetu ya Tanzania imearibika kuanzia Mzee wetu Mwinyi mpaka JK,Hakuna mwenye hafadhali.hii system ni sawa na Mgonja wa ukimwi hata uumpe madawa vipi lakini mwisho wake tunaujua wote.Ili nchi yetu iweze kuingia ktk kundi la nchi zinazoendele nilazima sisi vijana tuungane tuwang'oe hao wazee wakapunzike nyumbani tunashukuru kwa mchango wao lakini hawawezi kuleta maendeleo ninayoyataka mimi na wewe kijana wa karne 21.
Quote
 
 
+4 #6 2010-05-17 13:21
SIKUBALIANI NA MATAMSHI YA MZEE NINAYEMHESHIMU.ANAITWA MZEE RUKSA kwa sababu enzi zake kila kitu kilikuwa ok;hakukuwa na utaratibu(in latin-condranaturam).Tulishuhudia na hyper inflation(shili ngi ilikuwa kama takataka,ilishu ka thamani kupita kawaida).Hakuna mtu mwema ndani ya C.C.m.
Quote
 
 
0 #5 2010-05-17 09:22
Ama kweli nyani haoni ........
Wakati wa serikali ya awamu ya pili mawaziri wa serikali wanakamatwa airport na madawa ya kulevya na madini mbali mbali magwiji wa madawa hayo wanatoroshwa kutoka gerezani (wakina Kpt Aziz)matumizi ya Ki[NENO BAYA] ya fedha za uma kwenye mkutano wa mazingira wa Rio de Jeneiro.wizi wa mali za umma na kutokuwajibika kwa viongozi wa serikali na wafanya kazi wote ukiachilia mbali hakuna aliyejisumbua kukusanya kodi(au walikusanya lakini hazikufika serikalini) na kwa taarifa ni kipindi hicho ambacho tulianza kushuhudia viongozi wa serikali na mashirika ya umma wakijenga ma palace na kununua magari ya kifahari achilia mbali maamuzi mazito ya serikali yanatoka kwa wake za viongozi.Muulizeni Mzee Mkapa uozo alioukuta Ikulu.Tunakuheshimu Mzee Mwinyi Lakini acha hizo
Quote
 
 
+4 #4 2010-05-16 18:52
mzee Ruksa anaweza kuwa yupo sahihi kuwa wakati wake rushwa haikuwepo IKULU ila huku chini zilikuwepo japo ni ndogondogo siyo "grand corruption" tunayoiona sasa ya Viongozi wakuu kuingia mikataba ya kunyonya nchi(Overstated and fake government contract)

Tofauti kubwa ni kuwa Mwinyi alipata urasi chini ya CC iliyokuwa ikifanya kazi chini JK Nyerere. Hivyo hakuwa na deni la kulipa fadhila. Awamu ya nne imejaa watu waliokuwa na uchu wa madaraka ili kujilimbikizia mali hivyo kila opportunity inayotokea ya kufanya jambo la maendeleo viongozi wanapiga mahesabu kuwa "Mimi nitanufaikaje?".

Kama mwalimu angelikuwa hai leo hii watu kama kina Chenge RA, EL wasingekuwa tu viongozi, bali wananchama wa CCM.

Kikwete njia aliyopatia urais inamfanya kuwa vigumu kuwashughulikia watu hawa japo yeye binafsi huenda ana nia njema na ya dhati ya kuendeleza Taifa. Hili liwe funzo Kwa watanzania kuwa Public Office should not be used fro personal gain.
Quote
 
 
+7 #3 2010-05-16 11:11
Kitu muhimu ni kujua kuwa Raisi Kikwete amefika mwisho wake wa kufikiria nini cha kufanya kututoa hapa tulipo ili mtanzania wa kawaida angalao aishi kwa dola 2 kwa siku. Hajui mwenzake aliyepita aliwezaje kukusanya toka bil 36 na kufikia dola bil 300 na zaidi akitoka madarakani. Ni Raisi wa aina gani asiyekuwa na ufahamu wa mambo ya kawaida? Ni raisi gani anayetegemea kuongoza nchi kwa ushauri wa WAPAMBE?

Sishangai sana kwani Mwalimu alitujulisha mapema ila tulipenda tabasamu la kikwete zaidi ya ushauri wa Mwalimu.

Ushauri wangu ni kumwekea upinzani unaofikia nusu ya bunge ktk uchaguzi ujao, tutakuwa na uwezo wa kumtoa madarakani kwa njia ya kura za wengi kwa kutokuwa na imani naye.
Quote
 
 
+4 #2 2010-05-16 07:54
Mhe. Rais mstafu Mwinyi atanshangaa mengi tu si hili la rushwa peke yake. Aliishangaa pia hotuba ya Kikwete kwa wafanyakazi.Nina hakika alishangaa pia Kikwete aliposaini sheria batili kwa mbwembwe. Hata mipasho ndani ya CCM aliishangaa pia alipokuwa mwenyekiti wa kamati ya usuluhusishi ya CCM, kamati ambayo haikufankiwa kuondoa makundi yanayokimaliza chama hiki kikongwe. Nimkumbushe Mzee wetu tu kuwa Kikwete aliinia madarakani kwa rushwa ni lazima aikumbatie rushwa ili imuingize madarakani kwa awamu ya pili tena.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner