MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari Mkakati wa kuwang'oa Sitta, Makinda waiva
BOOKMARK THIS PAGE
Mkakati wa kuwang'oa Sitta, Makinda waiva  Send to a friend
Saturday, 01 May 2010 22:32

*Mpambe wa kigogo CCM akamatwa akigawa rushwa Songea
Sadick Mtulya
MKAKATI uliosukwa kuwang’oa baadhi ya wabunge katika majimbo yao unaodaiwa kusukwa na kigogo mmoja ndani ya CCM, umeanza kutekelezwa, imebainika.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa mpango huo una lengo la kuwaondoa baadhi ya wabunge wanaonekana ni kikwazo kwa kigogo huyo ndani ya bunge kufanikisha malengo yake, ili bunge lijalo liwe na sura mpya.
Niongoni wa wanaotakiwa kungolewa ni akiwemo Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Naibu wake, Anna Makinda pamoja na wabunge wengine.

Tayari mpango huo umeaanza kutekelezwa kwa kuwawekea wapinzani katika majimbo yao ambao wana uwezo wa fedha na wengine wanawekewa wapinzani wawili au zaidi ili kuhakikisha wanashindwa katika kura za maoni ndani ya CCM.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili unaonyesha kuwa tayari wabunge hao akiwamo Spika Sitta wamegundua hujuma hiyo na sasa wanajipanga kupambana na watu hao.

Hata hivyo, wabunge hao wameaamua kulifikisha suala hilo kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa CCM kuomba wahakikishiwe kama hujuma hizo zina baraka ya chama.

Taarifa zinasema kuwa mmoja ya wabunge hao alimfuata Rais Kikwete wakati wa mkutano wa 18 wa bunge mjini Dodoma mbele ya wabunge waliokuwa wameudhuria kwenye hafla ya jioni kuhoji kama chama kinajua mkakati huo.

Inadaiwa kuwa Mbunge huyo alimuuliza Rais Kikwete kana ni kweli kuna watu wametumwa na chama wakagombee ubunge kwenye majimbo wanayowakilisha, ili wasigombane.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa baada ya swali hilo, Rais Kikwete alishtuka na kulazimika kwendakwenye kipaza sauti ili wabunge wote waliokuwepo na kusisitiza kwamba, hajamtuma mtu yoyote majimboni.

Akizungumza  na Mwananchi Jumapili jana, Spika Sitta alikiri kusikia kuwepo kwa taarifa za mpango wa kung’olewa pamoja na Makinda na baadhi ya wabunge.

Hata hivyo, Sitta alisema mkakati huo ni sehemu ya mapambano ya siri yanayoendeshwa chini kwa chini dhidi yao.

“Pamoja na kwamba nipo jimboni hivi sasa, nimesikia kuwa mimi, Makinda na wabunge kadhaa tung’olewe,” alisema Sitta na kuongeza:
"Lakini yote haya ni sehemu ya mapambano ya siri yanayoendeshwa chini kwa chini dhidi yetu”.

Sitta alifafanua kwamba, mpango huo umewekwa dhidi yao kutokana na utendaji wao bungeni na kwamba wataendelea kupambana na hali hiyo.

“Kutokana na utendaji wetu bungeni, mimi na Naibu Spika tulijua hili  litajitokeza, lakini tutendelea kupambana na hali hii,” alisema Sitta.

Sitta alisema pamoja na mambo mengine wananchi pamoja na wana-CCM ndiyo watakaoamua hatma yao na si vinginevyo.

Alisema walioanda mpango wa kuwang’oa  ni watu wenye ajenda ya chuki na gadhabu ambazo hazina msingi wowote katika maendeleo ya nchi.
Sitta alibainisha kuwa pamoja na watu hao kutumia fedha nyingi, hawatafanikiwa.

“Hawa watu wana ajenda ya chuki na gadhabu ambazo hazina msingi wowote katika maendeleo ya  nchi,” alisema Sitta.

Sitta alijitapa kuwa hana wasiwasi na nguvu zinazotumika kumg’oa na kusititiza kwamba, atashinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

“Siku zote wananchi wanaangalia jinsi Mbunge alivyosaidia katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo yao pamoja na ya taifa. Hata  watumie fedha kiasi gani, mimi sina wasiwasi na  nitashinda,” alisema.


Sitta aliwaonya watu wanaotaka kumng’oa kuwa majibu ya jinsi anavyokubalika wangeyapata kupitia taasisi ya utafiti wa Demokrasia na Elimu nchini(Redet) kama ingefika kufanya utafiti katika jimbo lake.

 “Bahati yao utafiti wa Redet haukupita katika jimbo la Urambo Mashariki, wangepata majibu yao na wangejua mimi ni nani,” alisisitiza Sitta.

Juhudi za kumpata Makinda hazikuza matunda alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mchinga(CCM), Mudhihir Mudhihir ambaye ni mmoja wa wabunge waliotajwa kuwa walengwa wa mpango huo wa kung’olewa, alisema katika uchaguzi waamuzi ni wananchi.

“Katika jimbo la Mchinga wapo wagombea wanane ambao wameletwa, lakini ninachosema ni kwamba, wananchi ndio waamuzi katika uchaguzi wowote,” alisema Mudhihir

Mbunge huyo alisema pamoja na kwamba yupo tayari kupambana nao, lakini katika kupata ubunge hakuna ujanja na kwamba wote walituomwa kwa ajili ya kumuhujumu wataumbuliwa na Mungu.

“Mimi nitagombea na nipo tayari kupambana nao, lakini, naamini Mungu atawaumbua tu kutokana na nia zao mbaya,” alisema Mudhihir .

Kutoka Ruvuma,  Joyce Joliga, anaripoti kuwa
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Ruvuma inamshikilia mpambe wa mmoja vigogo wa (CCM) baada ya kukutwa akigawa rushwa kwa mabalozi 50 wa Kata ya Majengo, Songea mjini.
 
 Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kata ya Majengo, ambako mpambe huyo  (jina tunalo) alikamatwa akiwa nyumbani kwa mmoja wa wajumbe wa shina pamoja na mabalozi 50 kwa lengo la kuwapa Sh 2,000 kila mmoja.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma, Daudi Masiko alikiri kuwepo kwa tukio na kwamba taarifa kamili itatolewa kesho.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #21 2011-08-16 13:37
siasa ni kilimo....unapolima hasa kama hutumii njia ya umwagiliaji kuna uwezekano wa kuvuna au kutovuna....hizi ni siasa tu na mkwara bubu.wananchi ndio watajua wamchague nani na wamng'oe nani.
Quote
 
 
0 #20 2010-05-14 07:00
JAMANI MAADIMINISTRATO R WA KWENYE IZI COMENT WAKO MAKINI KWELI UYO JAMAA NO 12 APO JUU AMEMTUKANA KIONGOZI WETU UONGOZI UMEONA ??????
Quote
 
 
0 #19 2010-05-13 12:09
hapo ulipoandika NENO BAYA mimi niliandika naukoti huo mstari"kama kuna chi.z.i kama huyo waukweli"
Quote
 
 
0 #18 2010-05-13 12:01
umesema tuhakikishe tunatumia rugha safi na ya kistaarabu... sawa sisi wastaarabu tunekuelewa vipi umemuelewaje huyo anayejiita "WAUKWELI" soma coment # 12... ni vyema hizi comments ukawa unazipitia ili kama kuna [NENO BAYA] kama huyo waukweli ametuma comments uweze kuziondoa....
Quote
 
 
0 #17 2010-05-12 08:59
[quote name="moody"]Administrator! !! ina maana neno hili ndio neno baya kuliko hilo no;12? =u.ji.ng.a. huu? in/quote]
Quote
 
 
0 #16 2010-05-12 08:56
Administrator!! ! umelala au unahusika na u[NENO BAYA] huu? ina maana hujaona no; 12 alivyojionyesha kwamba yeye Mwanaharamu?unashindwa kulifuta tukueleweje au huyapitii haya maoni?
Quote
 
 
+1 #15 2010-05-11 16:03
Wewe kijitoto cha juzi kiitwacho Caroline usijiingize kwenye mtego wa Lengai Mmasai mwenzangu tukipeana Loishollo yanaisha sasa wewe itakuwaje? Acheni kusumbua chama yetu CCM!
Quote
 
 
+1 #14 2010-05-11 15:37
Ha ha ha ha ha wewe unayejiita Lowasa ukimpa Lengai chapa atakupigia kura.Yeye ni Mmasai mwenzako.Hata mkipeana ndama tu yanaisha anakupa kura upate kula lakini nadhani kwa upande wa CCM umechelewa.Zege mmelikoroga wenyewe lazima mlimalize.Zege hailali.Nadhani pamoja na kujiuzulu mwaka ule Watanzania bado wana wasi wasi na wewe kuwa haujaacha "UFISADI" alafu ile laana ya Baba wa Taifa bado kwako haitafutika milele usijihangaishe na uongozi nchi hii.
Quote
 
 
0 #13 2010-05-11 15:13
Administrator tembelea maoni ya wasomaji bado kuna watu wanatumia lugha za [NENO BAYA] mfano angalia maoni namba 12 hapa chini. Tuwe wastaarabu jamani lugha kama hizi si za kiutu uzima, aibu watoto wetu wanapoziona mtandaoni.
Quote
 
 
+1 #12 2010-05-10 19:40
KIKWETE K.U.MA LA MAMAKE
Quote
 
 
0 #11 2010-05-10 16:55
Quoting LENGAI:
Mimi nimekwisha sema kuwa kila mmoja atakula urefu wa kamba yake.Kama ulikaa jimboni kuwadanganya wananchi wako utavuna ulichopanda.Kama wewe unamwaga mapesa ukitegemea Watanzania ni wale wa miaka ya 60. Nilishasema pesa zao msiwache kuzichukua lakini kura pigieni vyama vimgine sio CCM. Mlijionea wenyewe walivyo na dharau.Wanadai wameweka wafanyakazi wao wa akiba sasa sijui wanawalipa nini?.Kila anayefukuzwa anaajiriwa mwingine makubwa.Hao mnaosubiri wenzenu wafukuzwe ndio muajiriwe mnakula wapi?.


Wewe Bwana mdogo huna nidhamu, mimi nilikuwa Waziri Mkuu nikakubali kujiuzulu na ninaipenda CCM hadi kufa, kwa nini inahimiza watu wengine kupigia chama ya upinzani? Tafadhali usifanye kampeni kupitia forum hii, nimekuona na nitakushughulik ia.
Quote
 
 
-1 #10 2010-05-07 18:32
Viongozi wetu wanadhani majimbo ni mali yao ndo maana wakisikia kuna mtu anataka kupambana nao kwenye uchaguzi matumbo yanawaka moto.

Demokrasia kwao ni maneno tu lakini mioyoni mwao usultani/ufalme umekithiri. Hii habari ya kujifanya eti wao ni watendaji wazuri ndo maana inapangwa mikakati ya kuwang'oa haina mantiki hata kidogo. Wnananchi ndo wenye uwezo wa kupima utendaji wao na si kujipigia debe. Kama wangekuwa watendaji wazuri wasingeruhusu uozo wakati wa mijadala ya Richmond, EPA n.k. Wamefanikiwa kucheza sinema wakijifanya sterling wa kihindi. Shame on you - all bogus politicians!
Quote
 
 
-1 #9 2010-05-06 18:55
Mimi nimekwisha sema kuwa kila mmoja atakula urefu wa kamba yake.Kama ulikaa jimboni kuwadanganya wananchi wako utavuna ulichopanda.Kama wewe unamwaga mapesa ukitegemea Watanzania ni wale wa miaka ya 60. Nilishasema pesa zao msiwache kuzichukua lakini kura pigieni vyama vimgine sio CCM. Mlijionea wenyewe walivyo na dharau.Wanadai wameweka wafanyakazi wao wa akiba sasa sijui wanawalipa nini?.Kila anayefukuzwa anaajiriwa mwingine makubwa.Hao mnaosubiri wenzenu wafukuzwe ndio muajiriwe mnakula wapi?.
Quote
 
 
+2 #8 2010-05-05 23:28
Gazeti la mwananchi kuweni makini, vinginevyo mtakuwa watumwa wa wanasiasa na kauli zao pana zilizojaa utata. Mtabaki kuwapigia kampeni badala ya kumsaidia mwananchi awaelewe wanasiasa ili ajue wa kumchagua.

Hivi hao akina Sitta, Makinda wana leseni ya kukaa kwenye majimbo yao hadi lini? Kwa nin wahoji uhalali wa watu wengine kugombea majimboni mwao? Hawana hata aibu kuongea hadharani eti watu wametumwa kuja kuwang'oa ili kufanikisha malengo ya mafisadi, kwani demokrasia ni nini kama hawataki ushindani?
Haya na huo ufisadi wanaojifanya wanapingana nao ni upi, maana kila atakapoongea Sitta anasema mafisadi wanafanya njama wamng'oe jimboni kwake. Inamaana kila anayegombea amekuwa fisadi? Labda neno fisadi limebadili maana yake atuambie vizuri lakini sio kulitumia katika kujitangaza.

Na nyie waandishi na wahariri kuweni makini jamani, msituchanganye wasomaji na siasa zenu. Hili wala halihitaji elimu kubwa kama za kiwango cha shahada kulielewa.
Quote
 
 
0 #7 2010-05-05 09:53
huyo sita na makinda waache woga, kama hawajatimiza ahadi zao walizowaambia wananchi its too late waache watu waje mjimboni kama perfomance yako nzuri iweje uweweseke? pambana
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner