Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Wananchi wamiminika ofisi za Nida Moshi, watoa ombi kwa Serikali ya Tanzania

Wananchi wakisubiri kupata Huduma,katika Ofisi za Nida zilizopo KDC, Mkoani Kilimanjaro. Picha na Florah Temba

Muktasari:

  • Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema ikifika Desemba 31, 2019 laini za simu za mkononi ambazo zitakuwa hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitasitishiwa huduma. Ili usajili laini kila mmoja anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa.

Moshi. Wananchi wameendelea kufurika katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) Mkoa wa Kilimanjaro kusaka vitambulisho hivyo ili kuwawezesha kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekwisha kusema laini zote za simu ambazo ikifika Desemba 31, 2019 zitakuwa hazijasajiliwa zitafungiwa.

 Leo Jumatatu Desemba 23,2019, Mwananchi limepita ofisi za Nida wilaya ya Moshi, zilizoko eneo la KDC ambapo imeshuhudia idadi kubwa ya wananchi wakiwa kwenye foleni wakisubiri huduma huku wakiomba muda wa usajili uongezwa.

Mmoja wa wananchi waliokuwa kwenye foleni, Remistoni Shao amesema ameanza kufuatilia kitambulisho hicho tangu Novemba 2019 na bado hajakipata jambo limekuwa likimpa usumbufu wa kufuatilia mara kwa mara ili kupata Namba.

"Nimeanza kufuatilia hiki kitambulisho toka Novemba na sasa ninachofuatilia ni namba ya kitambulisho hicho ili kuepuka kufungiwa laini yangu ya simu naiomba Serikali iongeze muda," amesema Shao.

Naye Catherine Samu amesema ipo haja kwa Serikali kuongeza muda na kurudisha huduma kwenye ofisi za kata ili kurahisishia watu kupata huduma na kuwapunguzia gharama za kuvifuatilia katika ofisi za Nida zilizoko KDC.

"Watu wanatoka mbali, wanatumia gharama kuja mpaka hapa, tunaomba Serikali iongeze muda na ikiwezekana huduma hizi zitolewe ofisi za kata," amesema

Akizungumzia malalamiko hayo, Ofisa usajili Nida Mkoa  wa Kilimanjaro, Abubakari Karinga amesema ucheleweshaji wa namba za vitambulisho hivyo unatokana na maombi kuwa mengi na uhitaji kuwa mkubwa.

"Wengi wanaolalamika kuchelewa kwa namba zao za vitambulisho vya Taifa ni kwamba unakuta maombi ya wananchi ni mengi na uhitaji ni mkubwa kwa wakati mmoja lakini wengine unakuta alisajiliwa lakini maombi yake yalikuwa na matatizo wakati wa kukamilisha usajili wake," amesema Karinga