Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yasomba na kuua wawili Dar

Muktasari:

Mvua zilizonyesha juzi na jana zimeharibu miundombinu jijini Dar es Salaam na kuua watu wawili                                                                                                          

Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Kiluvya, Aidan Kitare amesema tathmini iliyofanywa jana hadi leo Ijumaa asubuhi kufuatia mafuriko yaliyotokea jijini hapa, imebaini watu wawili wamekufa, nyumba tatu zimebomoka eneo la Kiluvya B

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Kitare amesema watu waliokufa ni Issa Ally(28) na Tedy Nolasco (8) na mwili wa Tedy umepatikana usiku wa kuamkia leo.

"Tumeuhifadhi mwili Hospitali ya Tumbi na watu ambao nyumba zilibomoka na kuingiliwa maji tumewapa hifadhi,” amesema.

Amesema bado wanaendelea kutafuta mwili wa Issa ambao bado haijapatikana.

Amesema uharibifu wa miundombinu kwa maeneo yote ya Kiluvya watatoa baadaye lakini barabara nyingi zimeharibika kwa kukatika.

"Taarifa kuhusu daraja la Kiluvya kwa sasa linapitika vizuri bila wasiwasi," amesema.

"Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wa Kiluvya pamoja na Watanzania kuwa makini wapitapo karibu na kingo za mito na madaraja lakini zaidi ya yote tuwachunge watoto."