Uzinduzi tovuti za halmashauri kuchochea maendeleo-DC

Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Saada Malunde

Muktasari:

 

  • Malunde alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua tovuti ya halmashauri hiyo itakayokuwa ikitumika kufahamisha jamii mambo mbalimbali yanayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya wilaya.
  • Ofisa habari wa halmashauri hiyo, Jonathan  Xavery alisema tayari wameshatoa mafunzo kwa maofisa habari na  wachambuzi wa mifumo ya kompyuta 35 kutoka mikoa ya  kanda ya ziwa ambayo ni Kagera, Mara , Mwanza, Shinyanga na Simiyu.

Biharamulo. Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Saada Malunde amesema kuanzishwa kwa tovuti za kila halmashauri kote nchini kutasaidia kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika nyanja mbalimbali.

Malunde alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua tovuti ya halmashauri hiyo itakayokuwa ikitumika kufahamisha jamii mambo mbalimbali yanayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya wilaya.

Ofisa habari wa halmashauri hiyo, Jonathan  Xavery alisema tayari wameshatoa mafunzo kwa maofisa habari na  wachambuzi wa mifumo ya kompyuta 35 kutoka mikoa ya  kanda ya ziwa ambayo ni Kagera, Mara , Mwanza, Shinyanga na Simiyu.

 “Tovuti yetu itajulikana kwa jina la www.biharamulodc.go.tz na kila kitu kitakuwa kikionekana kila kinapofanyika kwa wale watakaofungua muda wa tukio,”alisema