Uopoaji kivuko Mv Nyerere wafikia asilimia 96

Kivuko cha Mv Nyerere kinakaribika kuegeshwa katika pwani ya kisiwa cha Ukara kutokana na juhudi za kukivuta zinazoendelea kufanywa hivi sasa
Muktasari:
- Shughuli ya kukivuta kivuko cha Mv Nyerere hadi nchi kavu inaendelea vizuri baada ya hapo kitakabidhiwa kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa)
Dar es Salaam. Kamandi ya Wanamaji imesema shughuli ya uopoaji wa kivuko cha MV Nyerere kilichopinduka Alhamisi iliyopita imekamilika kwa asilimia 96.
Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji, Richard Makanzo akizungumza leo kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoka Ukara, alisema kinachofanyika kwa sasa ni kutoa maji ndani ya kivuko hicho kabla ya kukikabidhi kwa Temesa.
"Kazi hii inakaribia kukamilika na kinachoendelea sasa ni kutoa maji, tuna gari za zima moto zinazovuta maji ndani ya kivuko," alisema.
Soma zaidi: