Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spika aagiza Kubenea asakwe, Zitto afikishwe mbele ya kamati

Muktasari:

  • Wabunge hao wawili wanatakiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kuhojiwa kuhusu kauli zao walizotoa

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu Lissu.

Pia  Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti                       

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.