Simbachawene awapa rungu Ma-RC, DC kutumbua

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawe

Muktasari:

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawe ambaye alisema lazima wafanye hivyo kwani ndiyo kazi waliyotumwa.

Dodoma. Serikali imebariki kazi zinazofanywa na wakuu wa mikoa na wilaya ikiwemo kuwatumbua na kuwashusha vyeo baadhi ya watumishi ingawa imekiri kuwa kuna baadhi ya maeneo kama binadamu hukosea.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawe ambaye alisema lazima wafanye hivyo kwani ndiyo kazi waliyotumwa. 

Simbachawene alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia ambaye alitaka kujua mamlaka za wakuu wa wilaya kuwanyanyasa wananchi zinatoka wapi.

Nkamia aliliambia Bunge kuwa, kumeibuka vitendo vya wakuu wa wilaya na makatibu tawala kuwanyanyasa wananchi kwa kisingizio kuwa wao ni marais wa wilaya wakati Tanzania ina Rais mmoja Dk John Magufuli.