Ripoti ya uchunguzi wa makontena ya mchanga kutua kwa JPM kesho

Ripoti ya mchanga wa dhahabu mezani kwa JPM

Muktasari:

  • Matangazo hayo kurushwa moja kwa moja.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli kesho, Jumatano atapokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Wananchi wanakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 asubuhi kutoka Ikulu jijini hapa.