Ripoti ya Tanzanite kukabidhiwa leo

Rais John Magufuli
Muktasari:
- Rais John Magufuli amewasili eneo la tukio na kinachoendelea ni wimbo wa Taifa
Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo anakabidhiwa ripoti mbili za madini ya almasi na Tanzanite taarifa ambayo inarushwa moja kwa moja kupitia luninga ya Taifa TBC.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefika Ikulu kushuhudia ukabidhiwaji wa ripoti hiyo akiwamo Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na mawaziri wengine mbalimbali.
Ripoti ya kamati hiyo iliyoundwa na Spika wa Bunge Ndugai, kuangalia mfumo wa uchimbaji udhibiti ,usimamizi na umiliki wa madini hayo ya vito.