RC Mtaka ajivua maendeleo Simiyu

Muktasari:

Mtaka aeleza mambo mbalimbali yanayofanyika katika Mkoa huo ikiwa ni pamoja na kilimo cha pamba na kuwa na akiba ya chakula ya kutosha


Simiyu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema mkoa huo umefanikiwa kukabiliana na njaa kwa kuwa wananchi wake wamehamasika katika kilimo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 8, 2018 katika uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa kilomita 49 uliowekwa na Rais John Magufuli.

Mtaka amesema katika Mkoa huo walijiwekea malengo katika kilimo cha pamba, msimu wa 2018 wamezalisha tani milioni 1.4, huku akibainisha kuwa wana akiba ya kutosha ya chakula.

Amesema mwaka wa fedha wa 2017/18, mkoa huo umepokea Sh1bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo sambamba na Sh11bilioni za ukarabati wa vituo vya afya na zahanati.