Polisi wamnasa kinara wa ujambazi Kanda ya Ziwa

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa katika maficho yake kijiji cha Nyanza wilayani Butiama pia alikutwa bunduki aina ya Short Gun Pump Action yenye namba za usajili TZCAR 65040 SPAS12-L-FRANCH SPA-BRESCIA.

Musoma. Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia mtu anayedaiwa kuwa kinara na kiongozi wa kundi linaoendesha vitendo vya ujambazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa katika maficho yake kijiji cha Nyanza wilayani Butiama pia alikutwa bunduki aina ya Short Gun Pump Action yenye namba za usajili TZCAR 65040 SPAS12-L-FRANCH SPA-BRESCIA.

Kamanda Ng’anzi amesema baada ya mahojiano, mtuhumiwa huyo aliwaonyesha polisi eneo wanakoficha silaha ambapo bunduki nyingine aina ya Minifrale PAT yenye namba 986828 ilipatikana.

Amevitaja  vitu vingine vilivyokutwa kwenye maficho hayo ni sare moja inayofanana na za Jeshi la Wananchi (JWTZ), mashuka ya hosptali, nguo mbalimbali za kike na kiume zikiwemo vitenge doti tatu, pleti namba za magari zenye usajili STL 4531 na STL 2733 na nyingine ya pikipiki yenye usajili MC 760 AJS.