Nape ampa tano Rais Magufuli

Muktasari:

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi iliyofanywa na tume ya uchunguzi wa sakata la mchanga.

Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi iliyofanywa na tume ya uchunguzi wa sakata la mchanga.

Nape anaungana na baadhi ya wabunge ambao pia wamempongeza Rais Magufuli kutokana na kazi aliyofanya kupitia tume hiyo.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Nape ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Machi mwaka huu, ameandika, “hili la mchanga...big up!”

Baada ya kundolewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo nafasi hiyo sasa inashikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.