Mv Ukara kuanza kutoa huduma badala ya Mv Nyerere

Muktasari:
- Kivuko cha Mv Ukara kinatatajiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria na mizigo midogo midogo kati ya kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara na Bugorola
Ukara. Kivuko cha Mv Ukara kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara na Bugorola.
Akizungumza leo Septemba 27, 2018 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 70 kitatoa huduma kwa muda wakati Serikali inatafuta ufumbuzi mwingine wa usafiri kati maeneo hayo mawili.
Waziri Kamwelwe ameyasema hayo alipokuwa akielezea hatua za dharura zilizochukuliwa na Serikali kukabiliana na changamoto ya usafiri baada ya kivuko cha Mv Nyerere kupinduka Septemba 20, 2018.
Awali, kivuko cha Mv Ukara kilikuwa kikitoa huduma ya usafiri katika visiwa ya Kitale, Kweru, Ilungwa hadi mwalo la Bukima Musoma vijijini mkoani Mara.
Kabla ya ujio wa Mv Nyerere Mv Ukara ndicho kivuko cha kwanza cha Serikali kilichokuwa kikisafirisha abiria kati ya visiwa vya Ukara na Ukerewe.
Tofauti na Mv Nyerere, kivuko cha Mv Ukara hakipakii gari wala mizigo mikubwa zaidi ya ile midogo ya mikononi.
Soma Zaidi: