Yamoto na Mwenge Jazz kunogesha sherehe za Muungano

Wanamuziki wa bendi ya Yamoto
Muktasari:
- Amesema kutakuwa na maonyesho ya makomandoo ambao watakuja na ladha mpya ikiwa na mambo tofauti na yale ambayo wananchi wameyazoea.
Dodoma. Bendi za Yamoto na Mwenge Jazz zitatumbuza katika sherehe za maadhimisho miaka ya 53 Muungano zitakazofanyika mjini hapa Jumatano ijayo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na ajira Jenista Mhagama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa leo.
"Wanafunzi wa shule za sekondari kwa mara ya kwanza watapamba sherehe za muungano kwa kuonyesha uzalendo na ukakamavu na utii kwa Rais wao, "amesema Mhagama.
Amesema kutakuwa na maonyesho ya makomandoo ambao watakuja na ladha mpya ikiwa na mambo tofauti na yale ambayo wananchi wameyazoea.
Amesema pia maadhimisho hayo, ambayo yataonyeshwa moja kwa moja na Televisheni mbalimbali, yataanza saa 1.00 asubuhi na kumalizika saa 6.00 mchana na mgeni Rasmi ni Rais Dk John Magufuli.