Waombwa kuchangia timu ya Taifa ya tenisi

Muktasari:

  • Timu hiyo ya walemavu ni wawakilishi pekee wa bara la Afrika kwenye michuano hiyo itakayofanyika nchini Italia kuanzia Mei Mosi mpaka 7.

Dar es Salaam. Wadau wameombwa  kuichangia timu ya  Taifa ya tenisi ya wenye ulemavu ili wakacheze michuano ya kombe la Dunia.

Timu hiyo ya walemavu ni wawakilishi pekee wa bara la Afrika kwenye michuano hiyo itakayofanyika nchini Italia kuanzia Mei Mosi mpaka 7.

Kocha wa timu hiyo Riziki Salum amesema leo wameanza maandalizi ya kushiriki mashindano hayo makubwa ambayo yatailetea heshima Tanzania.

"Vijana wameingi kambini hapa Gymkhana kwaajili ya kujiandaa na mashindano hayo, tuna changamoto ya baiskeli na vifaa vingine kwaajili ya mashindano hivyo ni vizuri wadau wakajitokeza kutuongezea nguvu," amesema Salum.