Vyama Arusha kushtakiwa kwa Nape

Waziri wa Michezo Nape Nnauye

Muktasari:

  • Maneno ambae pia ni Afisa Michezo Jijini Arusha, alisema tangu Julai mwaka jana aliwaandikia barua makatibu wakuu wa vyama vya michezo kuwasilisha nakala za usajili pamoja na safu ya majina ya usajili lakini hakuna hata chama kimoja kilichowasilisha nyaraka hizo.

Arusha.Msajili wa Vyama vya Michezo Wilaya ya Arusha, Benson Maneno amesema amepanga kuvishtaki vyama vya michezo wilayani humo kwa Waziri wa Michezo Nape Nnauye ili avifute kwa kile alichodai kukaidi agizo la usajili.

Maneno ambae pia ni Afisa Michezo Jijini Arusha, alisema tangu Julai mwaka jana aliwaandikia barua makatibu wakuu wa vyama vya michezo kuwasilisha nakala za usajili pamoja na safu ya majina ya usajili lakini hakuna hata chama kimoja kilichowasilisha nyaraka hizo.

"Kwa namna vyama vilivyokiukwa suala hili lazima tuwashtaki kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo kwenye kikao cha Kamati ya Michezo kitakachofanyika Aprili mwaka huu," alisema Maneno.