Messi ahukumiwa kifungo, anusurika jela

Muktasari:

  • Gazeti la El Espanol limeripoti kuwa mshambuliaji huyo wa Barcelona amepatikana na hatia ya kukwepa kodi yenye thamani ya pauni 3.5milioni katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.
  • Pia, alishindwa kuthibisha kuwa anapokea kiasi cha pauni 8.7m ikiwa ni haki ya matangazo.

Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 kwenda jela, lakini nyota huyo hatotumikia adhabu hiyo.

Gazeti la El Espanol limeripoti kuwa mshambuliaji huyo wa Barcelona amepatikana na hatia ya kukwepa kodi yenye thamani ya pauni 3.5milioni katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.

Pia, alishindwa kuthibisha kuwa anapokea kiasi cha pauni 8.7m ikiwa ni haki ya matangazo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya Hispania kifungo hicho cha miaka miwili kinaweza kubadilika, hivyo Messi hatoweza kwenda jela katika muda huo.

Baba yake Jorge pia amefungwa miezi 21, lakini adhabu hiyo ilipunguzwa hadi kubaki miezi 15, hata hivyo amelazimishwa kulipa fainali ya pauni1.7milioni.

Messi si mchezaji pekee wa Barca mwenye kesi ya kukwepa kodi wengine ni  Neymar na Javier Mascherano, ambao kesi zao zinaendele.