Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mhandisi wa Mv Nyerere atamani kusimulia ajali ilivyokuwa

Muktasari:

  • Mhandisi Charahani ni kati ya watu 41 walionusurika baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama ziwani Septemba 20,2018 na kuangamiza watu 227 wakiwemo watoto na akina mama.

Mwanza. Mhandisi wa kivuko cha Mv Nyerere, Agostine Charahani anaendelea vizuri, huku ikielezwa kuwa anatamani kumsimulia kila mtu tukio la ajali ya kivuko hicho.

Charahani aliokolewa baada ya saa 48 kupita tangu kivuko hicho kilipozama Septemba 20, 2018 na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 26, 2018, mmoja wa madaktari wanaomtibu Charahani aliyeomba hifadhi ya jina lake amesema mhandisi huyo amekuwa na shauku ya kusimulia tukio hilo lilivyokuwa.

Amesema kila anapoingia chumbani alimolazwa mhandisi huyo anaanza kumsimulia namna safari ilivyokuwa katika sehemu aliyokuwa amekaa wakati kivuko hicho kikizama.

"Mgonjwa wetu anaongea sana, yaani kila daktari akiingia tu, anaanza kusimulia mwanzo hadi mwisho," amesema daktari huyo.

Amesema mhandisi huyo hayupo chini ya ulinzi, akisema, “huyu jamaa mimi sijaona kama analindwa, basi kama yupo chini ya ulinzi, kiukweli siwezi kuelezea maana sijaona ofisa yoyote wa usalama, iwapo yupo na amevaa raia, labda."

Ofisa habari na mahusiano hospitali hiyo, Lucy Mogele amesema licha ya kutokuwa na utaalamu na masuala ya utabibu lakini macho yanaweza kutabiri na kuashiria hali ya afya ya mtu.

"Mimi naona yupo sawa maana namna anavyopiga soga, sidhani kama ana tatizo jingine na ndio maana daktari ameagiza kwamba apumzike hadi baadaye," amesema Mogele.