Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Peneza wa Chadema kuzungumza leo

Muktasari:

Peneza mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho kumekuwa na vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.

Dar es Salaam. Mbunge wa Chadema, Upendo Peneza amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya mbunge huyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kueleza atakachozungumza.

Peneza mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho kumekuwa na vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.

Mkutano huo umeitisha ikiwa ni siku moja kupita tangu mbunge wa Siha wa Chadema, Dk Godwin Mollel alipotangaza kuhamia CCM akiunga jitihada za Rais John Magufuli.

Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 15, Peneza amesema ‘’nitakuwa na mkutano na waandishi,”

Mwananchi lilipotaka kujua kama mkutano huo atautumia kutangaza kuhama, Peneza hakukubali wala kukanusha zaidi ya kusisitiza ‘’wewe njoo katika mkutano utaelewa nakwenda kuzungumza nini.”