Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe: Hakuna utaratibu wa kumsafirisha Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Muktasari:

  • Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa sasa hakuna utaratibu wa kumsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda Marekani au Ujerumani kutokana na ushauri wa madaktari wanaomtibu.

Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake.

Amesema baada ya awamu ya kwanza ya matibabu aliyoyapata katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7, ya pili inafanyika Nairobi, Kenya alipo sasa.

"Awamu ya tatu itaamua aende wapi ambayo itahusu mazoezi," amesema Mbowe.