Masaju awasilisha muswada wa marekebisho ya sheria

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju

Muktasari:

  • Masaju aliwasilisha muswada huo mbele ya kamati ya Sheria na katiba leo, mjini Dodoma.
  • Akizungumza mbele ya Kamati hiyo Masaju alisema sheria zinazopendekezwa kurekebishwa katika Muswada huo ni ya Bajeti, Sura ya 439 na Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura namba 264.

Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju leo amewasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za mwaka 2017, unaokusudia kufanya marekebisho katika baadhi ya sheria.

Masaju aliwasilisha muswada huo mbele ya kamati ya Sheria na katiba leo, mjini Dodoma.

Akizungumza mbele ya Kamati hiyo Masaju alisema sheria zinazopendekezwa kurekebishwa katika Muswada huo ni ya Bajeti, Sura ya 439 na Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura namba 264.

Alisema marekebisho hayo yanafanyika kwa lengo la kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo pamoja  na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya  zinazorekebishwa na zilizopo.