Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kivuko cha Mv Nyerere chaanza kuvutwa nchi kavu

Kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimeegeshwa katika meli kubwa ya mizigo ya Mv Nyakibalya ili kisipunduke wakati kikivutiwa nchi kavu katika eneo la mwalo la kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Picha na Peter Saramba

Muktasari:

  • Shughuli ya kukivuta hadi nchi kavu kivukocha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20 imeanza baada ya upepo mkali uliokuwa ukivuma katika Pwani ya gati ya kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara kutulia


Ukara. Hatimaye shughuli ya kukivutia nchi kavu kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20 imeanza.

Shughuli hiyo ilianza saa 5:21 asubuhi ya leo baada ya upepo mkali uliokuwa ukivuma katika Pwani ya gati ya kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara kupungua kasi.

Pamoja na mitambo maalum ya kuvuta na kunyanyua vitu vizito, kazi hiyo pia inafanywa na meli kubwa ya mizigo ya Mv Nyakibalya ambayo imekibana ubavu wa kulia kivuko hicho ili kisipinduke tena wakati kikivutwa.

Awali, shughuli hiyo ilikwama kuanza kutokana na upepo mkali kuvuma.

Mmoja wa wataalam wanaoshiriki operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko hicho ameiambia Mwananchi kuwa, kazi ya kukivutia nchi kavu chombo hicho inatakiwa kufanyika ziwa likiwa limetulia.

Tangu asubuhi ya leo wataalam wa uokoaji kutoka majeshi ya ulinzi na usalama wakishirikiana na wenzao wa makundi mbalimbali walikuwa wakiendelea na tathmini ya namna ya kukamilisha kazi hiyo bila kusababisha madhara makubwa kwenye chombo.

"Kama tungetaka tu kukiburuza (kivuko cha Mv Nyerere) nchi kavu kazi hiyo ingekuwa imekamilika siku nyingi zilizopita; lakini tunataka kukitoe chombo majini bila kusababisha madhara makubwa," alisema kamanda wa vikosi vya wazamiaji, Luteni Amos Nyondo.

Mtaalam huyo kutoka makao makuu ya Kikosi cha Jeshi la Majini jijini Dar es Salaam amesema wanafanya kila linalowezekana kupunguza uharibifu.

Ajali ya Mv Nyerere iliyotokea hatua chache kabla ya kutia nanga katika gati ya Bwisya kisiwa cha Ukara na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200 na wengine kuokolewa wakiwa hai.

Soma zaidi: