Jafo aelezea kuhusu Unicef

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo .

Muktasari:

  • Fedha hizo ni kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za elimu ya msingi, hususan mafunzo kwa walimu, wanafunzi, wazazi na walezi, kamati na bodi za shule, wenyeviti wa vitongoji na kutoa elimu ya  malezi na haki za msingi za watoto kupata elimu bora.

Dodoma.  Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imepokea Sh 308.6 milioni sawa na asilimia 64.8 ya Sh 475.9 zilizopangwa kutolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) hadi Juni 2015.

Fedha hizo ni kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za elimu ya msingi, hususan mafunzo kwa walimu, wanafunzi, wazazi na walezi, kamati na bodi za shule, wenyeviti wa vitongoji na kutoa elimu ya  malezi na haki za msingi za watoto kupata elimu bora.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo amesema kuwa kuna makubaliano kati ya Serikali na Unicef.

 Amesema fedha hizo zinatolewa kwa ajili ya kujenga uwezo na hazitumiki kwa ujenzi wa miundombinu ya shule.

Alikuwa akijibu swali la Oran Njeza, mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM) aliyehoji msaada wa Unicef wa mwaka 2014/15 katika halmashauri ya Mbeya ulilenga kuboresha maeneo gani.

Pia alitaka kujua kiasi na asilimia ngapi ya msaada huo ulitumika katika miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida.