Azory Gwanda, Fatma Karume wapewa tuzo

Muktasari:

Ni katika maadhimisho ya miaka mitano ya mtandao huo.

 

Dar es Salaam. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umetoa tuzo kwa mwandishi wa Mwananchi, Azory Gwanda, kwa juhudi zake katika kutetea haki za binadamu.

Mke wa Gwanda, Anna Pinoni, alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya mume wake ambaye mpaka sasa hajulikani alipo tangu alipotoweka Novemba 21 mwaka jana.

Wengine waliopewa tuzo hizo ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tangayika, (TLS) Fatma Karume na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSN) Abdul Nondo.

Tuzo hizo zimetolewa leo Aprili 28, wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya kuwapo kwa mtandao huo.

Gwanda, mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa akiripoti kutoka Kibiti, alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, Novemba mwaka jana.