DC agoma kupokelewa madawati

Muktasari:

“Siwezi kukubali upuuzi huu, nimeagiza yarudishwe haraka,” amesema.

 

Mufindi. Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amekataa madawati 400 yaliyokuwa yamesambazwe kwenye shule za msingi za Mji wa Mafinga kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango.

William amesema madawati hayo yamesambazwa kwenye shule mbalimbali za mji huo bila kukaguliwa.

“Siwezi kukubali upuuzi huu, nimeagiza yarudishwe haraka,” amesema.

Pia amemwagiza Mkurugenzi wa mji huo, Saada Mwaruka kumsimamisha kazi Ofisa Ugavi, Amelia Malidadi.

Mwaruka alipoulizwa kama ametekeleza amri hiyo ya mkuu wa wilaya amesema: “ndiyo tumetoka kikaoni, kinachofuatia sasa ni kwenda kutekeleza agizo hilo la mkuu na mambo mengine yatafuata.”