Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NYANZA: Bei ya sukari jijini Mwanza haishikiki, watu wageukia uji

Muktasari:

Mkazi wa Mabatini, Julius Ntebe alisema familia yake na za jirani zimegeukia uji usio na sukari kwa kuwa chai haiwezi kunywewa bila kiungo hicho. “Inasikitisha, lakini watoto wameanza kuzowea,” alisema.

Mwanza. Kufuatia bei ya sukari jijini hapa kuendelea kupanda hadi kufikia Sh2,800 kwa kilo moja kutoka kati ya Sh2,000 na 2,400 baadhi ya wananchi wamegeukia kufungua vinywa kwa uji usiokuwa na kiungo hicho.

Mwaka jana, Serikali ilitangaza bei elekezi ya sukari kuwa Sh2,000 lakini imekuwa ikipanda bila kuwapo kwa maelezo yoyote, licha ya uamuzi wa Serikali kuingilia kati na kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

Mkazi wa Mabatini, Julius Ntebe alisema familia yake na za jirani zimegeukia uji usio na sukari kwa kuwa chai haiwezi kunywewa bila kiungo hicho. “Inasikitisha, lakini watoto wameanza kuzowea,” alisema.

Mfanyabiashara wa duka la rejareja katika Mtaa wa Mahina, Elbia Mnangwa alisema wanalazimika kupandisha bei ya bidhaa hiyo baada ya wauzaji wa jumla kuanza kuuza mfuko wa kilo 50 kwa Sh122,000 kutoka Sh110,000. “Sukari imegeuka kuwa bidhaa adimu. Bei inaweza kuongezeka pengine hadi kufikia Sh3,000 iwapo itaendelea kuadimika,” alisema Mnangwa.

Patrick Masawe anayemiliki duka eneo la Igogo ambaye hata hivyo alikutwa akiuza bidhaa hiyo kwa Sh2,700 kwa kile alichoeleza kuwa ni mbinu ya kuvutia wateja, alisema sukari imeanza kuadimika ndiyo maana inauzwa bei ya juu.

Akizungmzia kadhia ya kupanda kwa bei ya sukari, Nuriath Shaaban, mkazi wa Mtaa wa Mkuyuni aliiomba Serikali kuweka mikakati ili kuhakikisha unakuwapo upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa ajili ya kukomesha tabia ya wafanyabiashara kupandisha bei kila wanapojisikia.

“Kwa nini Serikali haiweki mikakati ya kukomesha tabia ya sukari kuadimika na kupanda bei kila mara wakati inajua mahitaji halisi ya nchi?” alihoji Shaaban.