Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Auawa kwa risasi Kibiti

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga

Muktasari:

> Mauaji haya ni muendelezo wa vitendo kama hivyo ambavyo vimeanza zaidi ya miaka miwili iliyopita

Kibiti. Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yake saa 6 usiku, kisha kufanya mauaji hayo.

Alisema kabla ya kufanya mauaji hayo walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha kumpiga risasi mbili mume wake.

Mganga wa Kituo cha Afya Kibiti Dk Sadock Bandiko amesema Ndikaye amepigwa risasi mbili mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.