Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya kivuko Mv Nyerere yatajwa sababu gulio kudorora

Kivuko cha Mv. Nyerere kikiwa kimegeuzwa na kusimama wima leo mchana. Picha na Jovither Kaijage 

Muktasari:

  • Kila siku ya Alhamisi wakazi wa kisiwa cha Ukara hupanda kivuko kuelekea Bugolora ambako huwa na gulio, walizoea kwenda huko kwa kutumia kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018.
  • Leo gulio limefanyika lakini likiwa na idadi ndogo ya watu


Ukerewe. Gulio la Bugolora wilayani Ukerewe limekosa msisimko. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na idadi ndogo ya watu waliojitokeza katika gulio hilo ikiwa imepita wiki moja tangu kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere.

Kivuko cha Mv Nyerere kilizama Alhamisi Septemba 20, 2018, mita 50 kabla ya kutia nanga katika gati la kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara, huku baadhi ya waliopoteza uhai wakiwa wakazi wa Ukara waliokuwa wametokea gulioni Bugolora.

Gulio hilo hufanyika kila Alhamisi na wateja wengi hutokea katika kisiwa hicho, lakini leo hali ilikuwa tofauti.

MCL Digital leo Alhamisi Septemba 27, 2018 limetembelea gulio hilo sambamba na kupanda kivuko cha Mv Nyehunge ambacho leo wananchi wa Ukara walikitumia  kwenda katika gulio badala ya Mv Nyerere.

Mmoja wa wafanyabiashara katika gulio la Bugorola, Munyaga Marcel amesema kupinduka kwa Mv Nyerere ni sababu ya gulio kukosa wateja.

"Wateja wetu wengi wanatoka Ukara kwa sababu hawana gulio na mahitaji yao yote wanategemea kutoka gulio la Bugorola. Nadhani  bado wako kwenye maombolezo ya vifo vya ndugu zao," amesema Marcel

Mfanyabiashara mwingine, Neema Mafuru amesema  mauzo yake leo yameshuka zaidi ya nusu kwa kuwa wateja wake wengi ni akinamama, leo hawakutokea kwa wingi.

“Nauza mbogamboga na kama ujuavyo wateja wengi wa mbogamboga ni akina mama na leo hawajaja wengi kabisa, wapo wachache sana,” amesema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa kisiwa cha Ukara wamesema licha ya hofu inayotokana na ajali ya kivuko, wataendelea kusafiri kwenda na kurudi katika gulio hilo kwa sababu ndiko kunakopatikana mahitaji yote muhimu.

"Licha ya hofu inayotokana na ajali hii iliyotokea wakati wakazi wengi wa Ukara wakitoka kwenye gulio la Bugorola, bado tutaendelea kwenda gulioni kwa sababu ndiko tunakopata mahitaji kutokana Ukara kutokuwa na gulio," amesema Msafiri John

Kauli hiyo pia iliungwa mkono na Siwema Mariga aliyesema "Nikiwa na fedha nitaenda gulio la Bugorola kwa sababu ndiko tunakopata mahitaji.”

 Soma zaidi: