SMZ yaahidi kufanya marekebisho ya sheria zinazowakwaza wanahabari

Muktasari:

Balozi Seif amesema hayo leo (Jumatano) wakati akifungua mkutano maalumu kwa wadau na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa nyombo vya habari yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha uwandishi wa habari kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.

Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema Serikali ya Zanzibar (SMZ) ipo tayari kufanya marekebisho ya sheria ambazo zinawakwaza wanahabari katika utendaji wao wa kazi ili kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari visiwani humo.

Balozi Seif amesema hayo leo (Jumatano) wakati akifungua mkutano maalumu kwa wadau na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa nyombo vya habari yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha uwandishi wa habari kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.

Amesema kama kuna sheria ambazo ni kikwazo kwa waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao Serikali haitosita kupokea mapendekezo ambayo yatapelekea kufanyika kwa marekebisho ya haraka.

 “Kama kuna sheria ambazo zinawasumbua au kuwabana katika utekelezaji wa majukumu yenu basi tunaahidi nasi tupo tayari kuzifanyia marekebisho yatakayowapa  fursa nzuri ya kufanya kazi kwa ufanisi,” amesema Balozi.

Amesema Serikali itandelea kulinda uhuru wa vyombo vya  habari kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa tasnia hiyo katika masuala ya uboreshaji na uimarishaji wa misingi imara ya kazi za wanahabari.