Wachimbaji wa madini Kanda ya Ziwa kukaguliwa, kupewa elimu

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Magharibi, Yahaya Samamba alipokuwa akizungumzia mpango wa ofisi hiyo wa kutoa elimu kwa wachimbaji ili kupunguza matukio ya ajali migodini ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Mwanza. Ofisi ya madini Kanda ya Nyanda za Ziwa inatarajia kufanya ukaguzi wa leseni za uchimbaji na shughuli zote za madini katika eneo hilo, imeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Magharibi, Yahaya Samamba alipokuwa akizungumzia mpango wa ofisi hiyo wa kutoa elimu kwa wachimbaji ili kupunguza matukio ya ajali migodini ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Alisema tayari ofisi yake imekusanya Sh2 bilioni kati ya Sh5 bilioni zilizotarajiwa kupatikana kwa ajili ya kazi hiyo kupitia tozo za ada za leseni, vibali mrabaha na  ada za kijiolojia.

Ofisa Mfawidhi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Kanda ya Ziwa, Hamad Kallaye alisema uzalishaji wa dhahabu kipindi cha masika umeshuka kutokana  na wachimbaji kuogopa kuingia migodini kuhofia kuangukiwa na udongo.

Pamoja  na hofu inayotokana  na mvua, Kallaye  alitaja changamoto  nyingine kuwa ni teknolojia duni, mtaji mdogo wa kumudu gharama na  miundombinu ya maji, umeme  na barabara katika maeneo  yao.