Sitta arejea nchini kutoka Ujerumani kwa matibabu

Muktasari:

 Mmoja wa wanafamilia wa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali serikalini, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa hali yake inaendelea vizuri.

Dar es Salaam. Spika wa Bunge mstaafu, Samuel Sitta amerejea nchini kutoka Ujerumani alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya miguu.

Septemba mwaka huu, Sitta alikwenda nchini humo baada ya kusumbuliwa na tatizo hilo.

Mmoja wa wanafamilia wa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali serikalini, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa hali yake inaendelea vizuri.

 Hata hivyo mimi siyo msemaji wa familia,” alisema mtoa habari huyo.

Alipotafutwa mke wa Sitta, Margaret ambaye alirithi ubunge wa Urambo kutoka kwa mumewe, alisema alikuwa benki na asingeweza kuzungumza  na simu.