Majaliwa azungumzia kufutwa CDA Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu swali hili amesema ni kweli Rais Magufuli alitoa ahadi kadhaa ikiwemo ya uboreshaji wa mji wa Dodoma na ahadi ya kuhamishia makao makuu Dodoma.

Dodoma. Mbunge  Kunti Majala ametaka kujua kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ahadi ya Rais John Magufuli alipolamikiwa na wananchi wa Dodoma kuhusu suala la CDA na kuahidi kuwa ataifuta CDA baada ya kuchaguliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu swali hili amesema ni kweli Rais Magufuli alitoa ahadi kadhaa ikiwemo ya uboreshaji wa mji wa Dodoma na ahadi ya kuhamishia makao makuu Dodoma.

Amesema kwa kuwa Serikali imehamia Dodoma inatakiwa kuboreshwa sheria mbalimbali ikiwemo za CDA na kuachana nayo kwa kuwa kwa sheria yake hivi sasa huwezi kupeleka mwekezaji Dodoma.