MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
JK: Masauni kajimaliza mwenyewe  Send to a friend
Wednesday, 19 May 2010 23:15

MWENYEKITI wa CCM Rais Jakaya Kikwete, amepiga msumari wa mwisho kwa aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Hamad Yusuph Masauni, akisema alijimaliza mwenyewe kwa kutokuwa mkweli kuhusu umri wake na watu wasitafute mchawi.
 
*ADAI HATUA ALIYOCHUKULIWA KAMA YA NAPE, BENNO MALISA ASEMA NI USHUJAA KUWANG’OA VIGOGO
Leon Bahati, Iringa
 

Kauli hiyo ya mwenyekiti wa CCM taifa ilizidi kummaliza kijana huyo ambaye tayari alijikuta katika tuhuma nzito za kughushi umri ili achaguliwe mwaka 2008.  

Rais Kikwete aliweka bayana hilo mjini hapa wakati akifunga mkutano tete wa Baraza Kuu la UVCCM, ambao ulifanya vigogo wawili wa juu wote kutoka Tanzania Zanzibar, ambao ni Masauni na Naibu Katibu Mkuu Nassoro Moyo, kujiuzulu.

Mwenyekiti huyo wa CCM, awali katika hotuba yake hakutaka kuzungumzia kwa undani sakata hilo, lakini baada ya kumaliza aliruhusu maswali na ndipo baadaye akauliuza wajumbe:, "Hivi mlielezwa vizuri kilichomfanya Masauni ajiuzulu?"  

Baada ya swali hilo ukumbi ulipuka kwa wajumbe kusema:, "hatujuiii...hatujuiii...hatujuiii."

Jibu hilo lilimfanya Rais kuanza kufafanua kwa kifupi na kuwambia wajumbe:, " Kilichomponza Masauni ni kutokuwa mkweli kuhusu umri wake...Alikuwa na tuhuma za kughushi umri uliomwezesha kushinda uchaguzi mwaka 2008."

"Tulipochunguza ilibainika ni kweli alighushi, wakati wa uchaguzi alisema alizaliwa mwaka 1979, lakini ukweli alizaliwa mwaka 1973 na alianza darasa la kwanza mwaka 1979."

Rais Kikwete alisisitiza:, "Kwa hiyo hakuna aliyeonewa, aliyefitini na wala watu wasitafute mchawi katika hili. Hatua kama hii ilikwishafanyika kwa watu kama akina Nape (Nnauye)." Nape naye alienguliwa katika uchaguzi wa UVCCM uliopita.

Alisema taratibu za UVCCM mtu akishakuwa na umri wa zaidi ya miaka 31, hawezi kugombea nafasi kutaka kuchaguliwa kwani anakuwa amepoteza sifa inayohusika.

Mwenyekiti huyo wa CCM awali, aliwaonya vijana hao wa UVCCM kuacha magenge kwani watajimaliza wenyewe badala yake mambo yao yapatiwe ufumbuzi ndani ya vikao na taratibu za jumuiya na chama.

Mkuu huyo wa chama na nchi, alifafanua kwamba kama malalamiko yakipita katika njia na taratibu za chama ni rahisi kupatiwa ufumbuzi kuliko kuyaanika hadharani kama ilivyofanyika. 

Hata hivyo, Rais Kikwete alimfariji kijana huyo mpole na mzito kufanya maamuzi magumu na haraka, akisema kwakuwa ni makakamavu na mchapakazi atapangiwa kazi nyingine hapo baadaye.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewataka wana CCM kujiandaa kujibu mashambulizi ya wapinzani kuhusu tuhuma za ufisadi ambazo alisema anaamini, watazitumia kama mtaji wakati wa uchaguzi.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa UVCC ambaye anakaimu nafasi ya Masauni, Benno Malisa, alisifia maamuzi ya kung'oka vigogo wenzake akisema ni ishara ya jumuiya kukomaa.

Malisa alitamba kwamba kitendo hicho kimeonyesha ushujaa ndani ya UVCCM na ni ishara ya ukomavu na ukuaji wa jumuiya.

Kwa wiki moja sasa, UVCCM walianza kurushiana makombora ya tuhuma nzito ambazo zilimtaja Masauni kwamba alighushi umri, taarifa ambazo zilisambazwa kwa njia ya waraka katika maeneo mbalimbali.

Gazeti hili ndilo la kwanza kuandika kuhusu wingu zito lililokuwa limetanda na kugubika mkutano huo wa vijana, huku duru zake zake za kisiasa za kuaminika, zikiweka bayana kwamba ilikuwa ni lazima kung'oka ama Moyo au Masauni au wote wawili, kitu ambacho kimetokea.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 20 May 2010 22:18
 

Comments 

 
0 #36 2010-05-20 21:30
Huyo karithi kwa baba yake alipokabidhiwa tume ya uchaguzi zanzibar naye alidanganya!
Quote
 
 
0 #35 2010-05-20 18:42
Tunawasubirini October 2010
Quote
 
 
0 #34 2010-05-20 17:03
kama hao wako wengi tofauti yao ni kwamba wengine wanamulikwa kutokana na nafasi zao na wengine hawna umuhimu mkubwa so no one care
Quote
 
 
0 #33 2010-05-20 16:52
Acheni kubabaisha hizo zote ni fitina ndani ya uvccm, kijana Masauni kaonekana mchapa kazi na kuwabana walaji matokeo yake ndio hayo kwani tangu mwanzo mlikuwa wapi msijue umri wake?
Quote
 
 
0 #32 2010-05-20 13:52
Ni kweli maamuzi mazito ya kijana huyo mpole,ila ni mfano wa kuigwa kwa wengine sio wenye kugushi umri tu hata wenye kufisadi nchi yetu wanahitaji kuupisha umma msafi,Lakini ni vipi mheshimiwa umeshindwa toa hukumu zinazowahusu mafisadi?pia Inaonekana kijana wako ni muhusika wa kuchochea ghasia katika umoja wa vijana??hawa watoto wa vigogo wanasumbua nchi kwanini wasiige mfano wa Mwl J K nyerere??
Quote
 
 
0 #31 2010-05-20 13:42
VIPI CCM UCHUNGUZI KUHUSU MASAUNI UFANYIKE MWAKA WA UCHAGUZI?INA MAAN UVCCM HAIKO MAKII KABISA KWANI KOSA WALILOFANYA NI KUBWA NA HALIPASWI KUFANYWA NA JUMUIYA YA VIJANA MAKINI. KWANINI ACHAGULIWE NA WAKATI UMRI ULISHAPITA? ZAIDI YA UMRI KUNA JAMBO LINGINE LILILOKUWA LINATAFUTWA LABDA MTUAMBIE HILO JINGINE
Quote
 
 
0 #30 2010-05-20 13:26
msumeno uwendelee usiishie kwa masauni
Quote
 
 
0 #29 2010-05-20 13:24
wembe uliotumika kwa masauni basi utumike pia kwa wale wote waliodanganya kuhusu elimu zao.kuwe na msumeno
Quote
 
 
0 #28 2010-05-20 12:12
adminstrator mbona hatuwezi kusoma maoni yetu, hayafunguki.
Quote
 
 
0 #27 2010-05-20 11:42
tunatuma maoni lakini hayonekani hapa vipi? wakati tunatumia lugha ya kistaarabu?
Quote
 
 
0 #26 2010-05-20 11:29
Wakati mwingine CCM iwe makini na vijana wake kabla ya uchaguzi hii ni aibu kwa chama na inaweza kuleta makundi katika chama
Quote
 
 
0 #25 2010-05-20 11:27
ni vizuri wakawa wakweli kuliko kungoja watu wakuaibishe. Je kwa hili hakuna mashtaka maana ni udanganyifu. Sheria zinasemaje kwa hili. KWELI WIZI MTUPUUUUUUUU
Quote
 
 
0 #24 2010-05-20 11:06
kazi ya Ridhiwani na Baba ake imeonekana.kwa kuwadokeza tu ni kwamba; Ridhiwani ni kijana anayeandaliwa kushika madaraka katika hii nchi, na ili apewe hayo madaraka, Baba ake aliamua kumpa mtihani wa kumpima kama anaweza kufanya fitna zenye kuzaa matunda.Na ili kutimiza hilo, pengo likaonekana kwa bwana Masauni , limefanyika kwa umakini sana na hayo ndo matunda. Usishangae kuona Makamba anashadidia, wala kikwete akipigilia msumari, ilikuwa tu ni kuhitimisha jaribio la umafia wa dogo Ridhiwani.CCM fitna, bila hivyo huendi. KUWENI MACHO NA WAMAFIA SI WAZURI KATIKA MAENDELEO YA NCHI YETU.
Quote
 
 
0 #23 2010-05-20 11:03
Mheshimiwa Mwenyekiti wa ccm Taifa hongera kwa hotuba yako nzuri lakini punguza jazba kwenye hotuba zako.
Quote
 
 
0 #22 2010-05-20 10:47
Vijana tukitaka mapinduzi ya kweli ndani ya jamii ili tujiletee maendeleo endelevu lazima tuwe wakweli mbele ya jamii tusitafute shortcut ya maisha madhara yake ndio hayo yaliyowapata akina masauni na moyo!maendeleo ya kweli hayafikiwa kwa kusema uwongo mbele ya jamii watu wa sasa wana elimu ya kutosha hawadanganyiki pia ikumbukwe kuwa sifa mojawapo ya msomi ni kusema ukweli si kuidanganya jamii ya uvccm hao si wa kuachwa walivyo bali wanatakiwa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hiyo pia Rais hakuwa sahihi kusema watapangiwa kazi nyingine hao hafai kabisa hata huko watakakopangwa wataendelea na udanganyfu huohuo na kuliingizia taifa hasara kubwa baadaye tuwe makini kwani yeye hajui kuwa kusema uwongo ni kuvunja sheria?
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner