Man United yamgeukia kinara wa mabao Lyon

Muktasari:
- Manchester United imeingia sokoni kuwania saini ya wachezaji watatu akiwemo mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele ikitaka kumsajili katika dirisha dogo.
London, England. Ole Gunnar Solskjaer amekosa saini ya Erling Braut Haaland, lakini hajakata tamaa ya kuisuka Manchester United na sasa anatupia jicho kila pembe ya dunia.
Man United ilikuwa na matumaini ya kumsajili Haaland, lakini ndoto yao ilizimwa baada ya kinda huyo kujiunga na Borussia Dortmund.
Baada ya kupata ushindi mfululizo dhidi ya Solskjaer dhidi ya Watford, Newcastle United na Manchester City, Solskjaer anataka kusajili mshambuliaji na viungo wawili.
Man United inasaka mchezaji wa kiungo kwa kuwa haina uhakika kama nyota Paul Pogba ataondoka au atabaki Old Trafford.
Kocha huyo amemgeukia mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele mwenye miaka 23 ambaye amekuwa akitakiwa na klabu hiyo muda mrefu.
Dembele anatajwa kama ndiye mridhi wa Romelu Lukaku aliyetimkia Inter Milan. Awali, Man United ilikuwa na matumaini ya kumnasa Haaland.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga mabao 10 katika mechi 18 alizocheza msimu huu na amekuwa katika kiwango bora.
Pia kiungo Saul Niguez wa Atletico Madrid ameingia katika anga ya Man United ikiamini ni mchezaji bora wa kuziba pengo la Pogba.