Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola atema cheche Manchester City

Muktasari:

  • Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hajakata tamaa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England, baada ya jana kuvuna pointi tatu dhidi ya Sheffield United.

London, England. Pep Guardiola amesema timu yake imechukua muda mfupi kurejea katika ubora wake baada ya kuifunga Sheffield United mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Guardiola alisema Manchester City ilicheza kwa kiwango bora katika eneo la ulinzi na kumiliki mpira licha ya kucheza na timu ngumu.

Kocha huyo alisema ushindi huo unaongeza kasi ushindani katika mbio za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu dhidi ya washindani wao wakubwa Liverpool.

“Najivunia kuwa na timu imara kwa misimu kadhaa, wanacheza kwa kujituma naridhika na juhudi zao,” alisema kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich.

Kocha wa Sheffield United Chris Wilder alisema licha ya kufungwa, wachezaji walicheza kwa nguvu na juhudi za kutaka ushindi.

Alisema haikuwa kazi nyepesi kucheza na timu yenye idadi kubwa ya wachezaji nyota duniani na hawezi kulaumu kwa matokeo hayo.

“Timu yangu ni imara imepambana na kikosi bora na meneja wa kiwango cha juu duniani, kwa namna tulivyocheza ni vizuri tulipata nafasi za kufunga lakini hatukuzitumia,”alisema Wilder.

Sheffield itacheza mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool ambayo inasaka kwa nguvu ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne alikuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kufunga bao la pili na kutengeneza jingine kwa Sergio ‘Kun’ Aguero.